ICJ yaiunga mkono Somalia katika mzozo na Kenya

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Uamuzi huo wa Jumanne unafungamanisha kisheria, inagwa mahakala hiyo ya Umoja wa Mataifa haina mamlaka ya utekelezaji.

Jopo la majaji 15 likiongozwa na jaji wa Marekani Joan Donoghue lilitoa uamuzi huo katika Peace Palace iliyoko Hague.

Kenya ilikuwa inataka, mpaka huo usalie jinsi ulivyo huku Somalia ikitaka ufanyiwe marekebisho.

Mahakama hiyo imesema kuwa Kenya ilikiuka makubaliano yote ambayo yalifikiwa na Somalia, mwaka 1979. Kenya kwa upande wake imekuwa ikisema kuwa eneo linalozozaniwa limekuwa himaya yake tangu mwaka huo.

Eneo hilo la bahari linalozozaniwa, lina ukubwa wa kilomita za mraba 100,000 sawa na takriban maili 40,000 za mraba.

Mikutano miwili ilifanyika mwaka 2014 kutafuta mwarubaini, lakini hakuna hatua iliyopigwa. Awamu nyingine ya mkutano iliyofuatia mwaka huo ilishindwa baada ya ujumbe wa Kenya kukosa kuhudhuria, bila kuufahamisha upande wa Somalia.

Somalia iliwasilisha kesi hiyo mahakamani mwaka 2014, baada ya kudai kuwa juhudi za kidiplomasia kutatua mzozo huo ziligonga mwamba.

Somalia haijawa na serikali imara tangu mwaka 1991 wakati utawala wa rais Siad Barre ulipopinduliwa, majaji wakisema kuwa suala hilo lilizingatiwa wakati wa kutoa uwamuzi huo.

Tayari Nairobi imeipa kampuni ya nishati ya Italia zabuni ya kuchimba mafuta na gesi katika eneo linalozozaniwa, hatua ambayo Somalia inapinga.

Mahakama hyo imesema kuwa mipaka kati ya kenya na Somalia inastahili kuzingatia mwafaka wa 1927 na 1933.

Mahakama hiyo imezikosoa Somalia na Kenya kwa kutoafikiana kuhusu mpaka unaozozaniwa.

Majuma mawili yaliyopita, Kenya ilifamhamisha katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress juu ya nia yake ya kujiondoa kutoka azimio la mwaka 1965 chini ya Mahakama ya Haki ya Kimataifa.

Mabunge ya Taifa na Seneti nchini Kenya, tayari yameshamuomba Rais Kenyatta kuwatuma wanajeshi iwapo sehemu yoyote ya Kenya ikiwemo eneo linalozozaniwa na Somalia litakabiliwa na kitisho, tamko ambalo limekosolewa na Mahakama ya Kimataifa ya ICJ. Peter Kagwanja ni mtaalamu wa masuala ya kidiplomasia.

"Mahakama ya ICJ ni mahakama ya kusuluhisha, sio mahakama ambapo haki hutekelezwa. Huwezi kusuluhisha mzozo wa majirani wawili ambao hawajazungumza. Unasuluhisha nini? Somalia haijawahi kupinga eneo hilo kuwa la Kenya, ili kuingilia himaya ya Kenya kwa kipindi kirefu,” amesema Kagwanja

Mwaka 2009, Kenya na Somalia zilisaini mwafaka, ulioidhinishwa na Umoja wa Mataifa kuhusu mipaka. Mwaka 2014, Somalia iliamua kusuluhisha mzozo huo katika mahakama ya ICJ, iliyoko The Hague. Kenya inashikilia kuwa mahakama ya ICJ haina mamlaka na uwezo wa kufanya uamuzi wa eneo linalozozaniwa.

Mataifa ya Kenya na Somalia yatalazimika kurejea kwenye meza ya mazungumzo kutatua mzozo huo ambao umedumu kwa kipindi cha miaka saba sasa.

Chanzo: DW Swahili
 
Ili uamuzi wa ICJ uwe valid, kenya pia lazima I consent kwamba mgogoro wao usuluhishwe nao. Kama upande mmoja umeenda, au kama ni maoni tu ya majaji, hakuna validity ya chochote.
 
ili uamuzi wa ICJ uwe valid, kenya pia lazima i consent kwamba mgogoro wao usuluhishwe nao. kama upande mmoja umeenda, au kama ni maoni tu ya majaji, hakuna validity ya chochote.
Kenya waliikimbia kesi mapema tu baada ya kuona watachapwa
 
Hamna uwezo wa kuigusa Tanzania
wait and watch,If somalia takes and we will do the same to Tanzania,sababu si mnasema ni fair mkichekaga hapa!!You as Tanzanians was supposed to be the first to support Kenya in this case,because even South Africa is supporting Kenya because if Somalia succeeds its going to affect the boundaries mpaka South!!!
 
Hamna uwezo wa kuigusa Tanzania
Alafu tena braza sisi wakenya hatuna neno sisi tukinyanganywa basi nasisi tutakiendea chetu pia,hehehehehe!! Is called a fair world this days,Somalia waliona hawatuwezi kivita wakaona watumie sheria!Nasi pia tukishindwa tutatumia sheria hio hio kwenyu,na nyinyi mjitayarishe kufanyia hivo Mozambique, Na mozambique ifanyie hivo SouthcAfrica,Alafu unajua nini the biggest looser atakuwa Tanzania mwishowe sababau ya Pemba island kweli naimeza mate!hehehehehe
 
Kwani ujui mombasa ni mali ya zanzibar hapo ndipo mnapo nichekeshaga .....labda mseme mkikasirika mtarudisha mombasa kwa wenyewe wazanzibar
 
Samahani lakini Una Umri gan kiongozi?
 
Kwani ujui mombasa ni mali ya zanzibar hapo ndipo mnapo nichekeshaga .....labda mseme mkikasirika mtarudisha mombasa kwa wenyewe wazanzibar
huyu jamaa ana point za kitoto saana nadhani ni vyema ukamuelewesha kuwa maamuzi hayo hayajafata kunyooka kwa mstari ila yalilenga sababu za kihistoria zaidi
 
wait and watch,If somalia takes and we will do the same to Tanzania,sababu si mnasema ni fair mkichekaga hapa!!You as Tanzanians was supposed to be the first to support Kenya in this case,because even South Africa is supporting Kenya because if Somalia succeeds its going to affect the boundaries mpaka South!!!
Hamna uwezo wa kushindana na Tanzania.hiyo Pemba haijawahi kuwa sehemu ya Kenya wala haitakuja kuwa sehemu ya kenya.nyie kwetu ni watoto wadogo.hamna uwezo wa kutusumbua.
 
Alafu tena braza sisi wakenya hatuna neno sisi tukinyanganywa basi nasisi tutakiendea chetu pia,hehehehehe!! Is called a fair world this days,Somalia waliona hawatuwezi kivita wakaona watumie sheria!Nasi pia tukishindwa tutatumia sheria hio hio kwenyu,na nyinyi mjitayarishe kufanyia hivo Mozambique, Na mozambique ifanyie hivo SouthcAfrica,Alafu unajua nini the biggest looser atakuwa Tanzania mwishowe sababau ya Pemba island kweli naimeza mate!hehehehehe
Haiwezekani hata mfanyaje hamna uwezo wa kufanya chochote.ile sehemu Somalia wanasema ilikuwa Yao.
 
Wenye wanasema haiwezekani ngojeni pia sisi tulithani Somalia haiwezi,kumbe kweli GDP makaratasi tuu! Poh
 
I stand with Kenya.
ICJ waende wakamzuie China kwenye bahari ya Kusini kwanza ndio waje kudeal na Kenya.
 
wait and watch,If somalia takes and we will do the same to Tanzania,sababu si mnasema ni fair mkichekaga hapa!!You as Tanzanians was supposed to be the first to support Kenya in this case,because even South Africa is supporting Kenya because if Somalia succeeds its going to affect the boundaries mpaka South!!!
What boundaries, u have nowhere to adjust on our side....... If think there is why don't u try to even mention it?!
 
Back
Top Bottom