ICC waondoka DSM na kuelekea Zanzibar!

Delegate

JF-Expert Member
Jan 4, 2012
331
201
ICC walikuwa wameweka ofisi zao Dar wameenda Zanzibar kushuhudia na kukusanya ushahidi wa kinachoendelea wam,eambata na Rais mstaafu wa Nigeria Goodluck Jonathan.

Sshida na matatizo ndio zinaanza hivyo na nafikiri hawatakaa muda mrefu inabidi warudi bara mapema manake huku ndio kutakuwa na shughuli pevu
 
Sikuwahi hata siku moja kuwapa watu weupe nafasi ya kuamini kuwa sisi Waafrika ni dhaifu, ni jamii ninamoishi inanilazimisha kuwapa wazungu advantage hiyo!
Kampeini miezi miwili amani tele, kupiga kura amani tele, kuhesabu kura amani tele. INAKUWAJE TUNASHINDWA KUIDHINISHA MATOKEO YALIYOKWISHA HESABIWA!!!!???
 
Shida na matatizo ndio zinaanza hivyo na nafikiri hawatakaa muda mrefu inabidi warudi bara mapema manake huku ndio kutakuwa na shughuli pevu

Kuna mdau alianzisha uzi juzi na mods waliupoteza huo uzi. Alikuja kwa aina hii;

Wana jamvi nawaomba tuweke utabiri wetu wa nani (ataburuzwa) kiongozi gani ataburuzwa icc mara baada ya uchaguzi mkuu?
Mimi nilichangia hivi.

Tanzania ina marais mbili.
1.Rais wa Tanganyika na Serikali ya Muungano
2.Rais wa serikali ya Zanzibar

Hawa wanaweza pata ile tuzo ya Mo au wanaweza kukabiliana na mashitaka huko ICC. Hiyo inategemea vipi watasimamia uchaguzi mkuu.

Uchaguzi mkuu ukiwa huru na wa haki, Kikwete atakwaa hiyo tuzo ya Mo Ibrahim kwa vile yeye ni mstaafu baada ya ukomo wa mihula miwili kama Katiba inavyotaka.

Uchaguzi ukitawaliwa na fujo na kutokea machafuko na maafa au matokeo yakichakachuliwa, yule mwanamama Fatou Bensouda wa ICC atapata kibarua.

Viongozi wengi wataambatanishwa kwenye mashtaka kutegemeana na nani ametoa amri gani ambayo italeta uvunjifu wa amani, unyimaji wa haki au uvunjifu wa haki za kibinadamu.

Ni mpaka pale yatakapotokea machafuko,maafa,majanga, uvunjaji wa haki za binadamu ndio tutaweza kusema nani ajiandae kwenda kumpa company Charles Tayler na Laurent Gbagbo.

Kwa sasa tusubiri uamuzi wa wananchi kupitia kura na tusubiri kuona umahiri wa Tume ya uchaguzi wa kusimamia uchaguzi huu. Haki ikitendeka hakuna ataeshitakiwa ICC.

Je haki itatendeka na kuonekana kuwa haki imetendeka?
 
Sikuwahi hata siku moja kuwapa watu weupe nafasi ya kuamini kuwa sisi Waafrika ni dhaifu, ni jamii ninamoishi inanilazimisha kuwapa wazungu advantage hiyo!
Kampeini miezi miwili amani tele, kupiga kura amani tele, kuhesabu kura amani tele. INAKUWAJE TUNASHINDWA KUIDHINISHA MATOKEO YALIYOKWISHA HESABIWA!!!!???
Mkuu mara zote wakati wa kupiga kura Tanzania ni amani tupu. Niliwashangaa wale waliokuwa wakidhani mabomu yatapigwa jana siku ya kupiga kura. Taabu uanza mara baada ya kuhesabu kura pale watendaji wanapojaribu kutangaza yasiyo halisia!
 
ICC walikuwa wameweka ofisi zao Dar wameenda Zanzibar kushuhudia na kukusanya ushahidi wa kinachoendelea wam,eambata na Rais mstaafu wa Nigeria Goodluck Jonathan.

Sshida na matatizo ndio zinaanza hivyo na nafikiri hawatakaa muda mrefu inabidi warudi bara mapema manake huku ndio kutakuwa na shughuli pevu
Wewe mwongo. ICC ni after the fact, siyo kabla hakijatokea.
 
Mkuu mara zote wakati wa kupiga kura Tanzania ni amani tupu. Niliwashangaa wale waliokuwa wakidhani mabomu yatapigwa jana siku ya kupiga kura. Taabu uanza mara baada ya kuhesabu kura pale watendaji wanapojaribu kutangaza yasiyo halisia!
Umenena kazi si kupiga kura bali kitakachotokea baada ya kupiga kura Tatizo watawala wa kiafrica wanafikiri wakipewa dhamana nchi zinakuwa zao.CCM Zbar haikuwahi kushinda ht siku moja ni ubabe tu.
 
Nashangaa sana mtu napoanzisha uzi akiwa na inner compulsion ya fujo itokee. . . .

Ilhali hata harufu ya baruti hawezi itambua. . . .
 
Sikuwahi hata siku moja kuwapa watu weupe nafasi ya kuamini kuwa sisi Waafrika ni dhaifu, ni jamii ninamoishi inanilazimisha kuwapa wazungu advantage hiyo!
Kampeini miezi miwili amani tele, kupiga kura amani tele, kuhesabu kura amani tele. INAKUWAJE TUNASHINDWA KUIDHINISHA MATOKEO YALIYOKWISHA HESABIWA!!!!???
Tell them, wanatafuta kila sababu ya kulianzisha.
 
Back
Top Bottom