Viongozi wa kiafrika pamoja na kufuta tongotongo lakini bado hawana tofauti yoyote na ma chief wa makabila yetu miaka ile ya giza.
Kitendo cha wao kukubaliana na kusaini mkataba wa Roma na kisha baadae kuanza kulalamika na kutaka kujitoa ni kitendo ambacho hakina tofauti yoyote na mikataba aliyokuwa anaingia chief Mangungo wa Msowero!
Kama viongozi wetu wa kiafrika wangekuwa na akili nzuri wangekuwa wanajadiliana na kushauriana namna ya kuimarisha demokrasia na utawala bora katika nchi zao badala ya kwenda kupanga mipango miovu dhidi ya wananchi wao kisha wanabaki kulialia mara tu wanaposhtakiwa ICC kwa ufedhuli wao.
Kutiki chikaka.
Nafikiri ni mila na desturi za kiafrika ndo tatizo, nafikiri mila za kiafrika zinapenda kujionyesha onyesha sana na ubabe ubabe fulani.
Mie hua nafanya fanya ka research ninapopata bahati kutembelea mjini katika miji ya watu.
1. Kwa asilimia yani 90% utakuta kijana mwafrika anatembea kibabebabe amatanua miguu, mikono na suruali kiunoni, saa kubwa kiatu kirefuu na miwani mieusi mikubwa hata kama kuna dondoka barafu.
2. Kwa asilimia 90% waafrika wanapenda kuishi kwenye miji mikubwa mikubwa hata kimsingi huo mji mkubwa kwake ni mzigo mkubwa sana.
Rudi nyumbani
1. Utakuta mtu analazimisha kujenga linyumba kubwaaaaaa hata kama kwenye nyumba hiyo ataishi pekee yake hajali, atahakikisha anajenga linyumba kubwa hata kufisadi afisadi.
2. Mtu unakuta anapenda gari kubwa kubwa si viongozi tu, hii ni kwa waafrika wote.
3. Jamani hapa mnisamehe, tunapenda wanawake wakubwa wakubwa wenye maumbile makubwa makubwa, sasa hadi tumewaathili baadhi ya kina mama na sasa wana pigania kujiongezea maumbile makubwa makubwa.
Hapa nataka kusema hivi, kimsingi nafikiri waafrika kwa sababu wenda ya tamaduni tunapenda ukubwa na kuvuta attention ya watu wengine kwa fenomenani ya vikubwa vikubwa. Kutokana na hiyo, ndo maana watu wanatafuta ukubwa ama uongozi kw gharama yoyote ile na akifika kule, ni ngumu kuuchia ukubwa naku achia attention anayopata itoweke.
Sasa hao, majamaa wanaona ICC ni kikwazo kwao kuendelea ku maintain vitu vikubwa vikubwa. Maana kimsingi, ili uwe mkubwa lazima uendelee kuwa madarakani, na kuendelea kuwa madarakani kimsingi hata uwe mzuri vipi watu watakuchoka na kuhasi na wakihasi ina maana itabidi uwa extinguish , na process ya kuwa extinguish is where ICC kicks in.