Bara la Afrika kwa sasa ndilo linaloongoza kwa kuzalisha marais wengi madikteta,sasa marais wa aina hiyo wanapoketi Addis Ababa na kutoa mwito kuwa wao wana uwezo wa kuendesha kesi hizo nchini mwao.
Hivi katika nchi za kidikteta zinaweza kuwa na mahakama zinazoweza kutenda haki kwa kutoa hukumu za haki kwa wale waliotenda makosa,bila kujali political power zao?!
Jibu la wazi ni kuwa hilo haliwezekani kabisa kwenye nchi zetu.
Hebu tuonyeshe mfano mmoja tu wa madaraka aliyopewa Waziri wetu wa habari wa kuchunguza,kushitaki, na kuhukumu yeye mwenyewe bila kutoa nafasi ya upande unaoshitakiwa kujitetea!!
Kwa mazingira hayo nawaomba ICC muendeleze uzi huo huo, wa kuwaburuza hawa viongozi wetu madikteta na kuwapeleka the Hague, ambako huko hakuna cha DPP, wala IGP, wala TISS wa kuweza kuzizima hizo kesi!!