mnyamiwono
JF-Expert Member
- Oct 7, 2012
- 708
- 71
Habari ndugu wanajamvi!
Naamini kabisa mko safi na imara kabisa katika ujenzi wa Taifa hili, hongereni saana!
Naomba sasa tujadili uzi huu kwa manufaa ya Taifa letu na Afrika kwa ujumla kama tulivyozoea kuimba Mungu ibariki Afrika ,Mungu ibariki Tanzania.
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa nyingi katika vyombo vya habari na kwa watawala wenyewe wa Afrika wakidai eti mahakama ya ICC inawaonea viongozi wa Afrika na inavyosemekana kuanzia kesho jumamosi na jumapili wanakutana addis ababa ,Ethiopia.
Moja ya ajenda muhimu ni kuujadili mkataba wa ROMA na kuona ni jinsi gani ya kujitoa kama wanachama wa ICC kwa ujumla wao.
Sasa hebu tujiulize watawala hawa wanaitakia mema Afrika ya waafrika kweli?
Mbona wanahofu na mahakama hii pasipokutueleza kuwa mahakama hii ilimuonea mtu Fulani au kiongozi Fulani wa Afrika?
Kagame, amseveni, Kenyatta, Mugabe, Albashiri ndio wanaoonekana vinara wa mpango huu, sasa tujiulize kuna nini nyuma ya pazia la utawala wao?
Hivi wanataka kutowajibika popote endapo watatenda makosa ya uvunjaji wa haki za kibinadamu katika nchi zao?,na pia kwa kufanya hivo watawaliwa watakuwa wanatendewa haki kweli?
Kwani kwa mtazamo wa kawaida ICC ni mtetezi wa wanyonge na wahanga wa vita vya kiutawala barani Afrika.
USHAURI WANGU:
Watawala hawa waachane na mjadala huo kwani hauna tija kwa watawaliwa wa Afrika,zaidi wajadili namna ya kufuta mikataba ya kibepari yenye kuiba maliasili kutoka Afrika ikiwemo Tanzania ili kuwaletea wananchi wao Ustawi katika maisha yao.
KARIBUNI WANAJAMVI!.