SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 6,995
- 11,502
Kuna hii dhana ipo vichwani mwa mashabiki wa Yanga kudhani Kocha wa Al Hilal Florent Ibenge anaenda kuilegezea Yanga ili ipate walau sare katika mechi ya Jumapili. Ngoja nikwambie kwa nini hilo ni gumu kutokea.
1. Al Hilal wanataka kumaliza group stage kwa alama nyingi inavyowezekana na bila kufungwa. Hapa kuna sababu tatu. Kwanza, ni kuhakikisha wanamaliza wakiwa wanaongoza kundi. Pamoja na kwamba sare inaweza kutosha kwao kujihakikishia kuongoza kundi ila asiwaamini sana Yanga kwenye hilo, wanaweza kukubaliana watoke sare wakawageuzia kibao mwishoni mwa mechi, awe makini sana.
Pili, kumaliza kwa point nyingi na kufika mbali kwenye mashindano ni kwa ajili ya CV binafsi ya Ibenge itakayombeba mwishoni mwa msimu. Tatu, wanataka wajiwekee rekodi zao wenyewe za kujivunia.
2. Al Hilal wana ukaribu na Simba. Simu moja tu kwa uongozi wa Al Hilal unafuta uwezekano wote wa Al Hilal kuilegezea Yanga labda kama simu hiyo ina ombi maalumu la namna hiyo ila sioni huo uwezekano.
3. Al Hilal lazima wajiulize nani ana uafadhali akija kukutana naye mbele ya safari, SM Algier au Yanga? Hili ni swali gumu ila wao ndiyo wanajua jinsi ya kulijibu.
Binafsi sioni kama Al Hilal wana vishawishi au sababu yoyote ya kuilegezea Yanga.