Ibada zarejea kanisa walimokutwa wakifanya mapenzi

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
430
998
Uganda. Waumuni wa Kanisa la Bunyonga, kaunti ndogo ya Kayonza wilaya Kayunga nchini Uganda ambapo mwanaume na mwanamke walikutwa wakifanya mapenzi katika madhabahu ya kanisa hilo, wamefanya ibada kanisani humo kwa mara ya kwanza baada ya kufanyiwa maombi ya utakaso.

Kiongozi wa Kanisa hilo, Aaron Komugisha, amesema timu ya makasisi na waumini wengine kutoka Kitimbwa wakiongozwa na Kiongozi, Dan Kisitu walifanya maombi maalum katika kanisa hilo ili kulitakasa.

Waumini katika kanisa hilo waliapa kutofanya ibada kanisani hapo mpaka pale litakapotakaswa baada ya mwanaume mmoja kukutwa akifanya mapenzi na mwanamke katika kanisa hilo Jumatano iliyopita.

Wapenzi hao ambao mwanaume ni mwanandoa mwenye watoto wawili huku mwanamke akiwa ni mtalakiwa walifikishwa kwa Mwenyekiti wa kijiji, George Kanda baada ya kukamatwa wakifanya tendo hilo ambapo aliwaandikia kesi.
“Tumerejesha ibada katika kanisa letu baada ya kuwa na siku ya kufunga na kufanya maombi. Sasa kanisa letu liko safi dhidi ya tendo lile la Kishetani ambalo lilifanyika,” alisema Komugisha.

Kiongozi msaidizi katika kanisa hilo, Esther Nakamate alisema,“tuanomba radhi kwa kila mtu. Tunawataka waje kanisani hapa na kuomba msamaha kwa kile walichokifanya na wasipofanya hivyo hatuwasamehe.”

CREDIT: MWANANCHI
 
mwanadamu anaweza kutakasa kanisa
 
Tendolao walilofanya

Halina tofauti na upokeaji sadaka nazo hupekelewa na hutakaswa kabla ya Matumizi

Kwasababu hua hazijulikani zimetoka wapi
 
Kuna watu wana roho ngumu hawaogopi Mungu, wanafanya mapenzi hata kwenye nyumba za ibada. Hawa ni wale waliozoea kufanyia mapenzi vichakani, uchochoroni, mitaroni na mapagarani. Kuna mmoja nilimtongoza akanikubalia, jirani kulikuwa na jengo moja la kuabudia lililotelekezwa alitaka tukanyanduane huko ndani nikamkatalia, nilipaheshimu pale japo paligeuka ni sehemu ya chapchap kufanyia faragha hiyo kwa wahuni wasio na hofu ya Mungu. Jamii ya pale ilipiga kelele wenye jengo hilo la kuabudia warudishe kufanyia ibada hapo kwani jengo hilo liligeuzwa na wahuni kuwa ni danguro huria. Siku hizi ibada zilisharudi na zinafanyika kama awali uhuni haufanyiki tena pale. Mashetani huwa hayana aibu
 
Back
Top Bottom