Ianzishwe vita- Rage.na mimi namuunga mkono | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ianzishwe vita- Rage.na mimi namuunga mkono

Discussion in 'Sports' started by Saint Ivuga, Jun 23, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,515
  Likes Received: 19,937
  Trophy Points: 280
  [TABLE="align: center"][TR][TD="class: headline, bgcolor: #ffffff"][/TD][/TR][TR][TD="class: headline, bgcolor: #ffffff"]Rage aapa kutokanyaga Kinshasa[/TD][/TR][TR][TD="class: headline, bgcolor: #ffffff"][​IMG][/TD][/TR][TR][TD="class: storyheader, bgcolor: #ffffff"][TABLE="align: left"][TR][TD][/TD][/TR][TR][TD="class: mwanacss, bgcolor: #b47c01"]Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage[/TD][/TR][/TABLE]MICHAEL MOMBURI, KINSHASA MWENYEKITI wa Simba, Ismail Aden Rage, ameapa kwamba timu hiyo haitakanyaga Kinshasa milele na wakipangiwa watajitoa kwani si sehemu salama na amesema watashtaki kwa Serikali ya Tanzania. Simba ilifungwa mabao 2-0 juzi Jumapili katika mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya DCMP ya hapa na kuondoshwa katika mchezo huo uliogubikwa na fujo za kila aina ndani na nje ya uwanja. Baada ya mchezo huo, maelfu ya mashabiki walivamia uwanja kwa lengo la kuidhihaki Simba jambo ambalo lilifanya askari wa usalama kuwatuliza wachezaji na viongozi kwenye benchi la ufundi na kuwazunguka kuwaepusha na fujo hizo zilizodumu mpaka usiku. Dakika chache baadaye wachezaji hao walisindikizwa tena hadi vyumba vya kubadilishia nguo na kutulizwa kwa zaidi ya saa moja hadi hali ilipotulia, lakini hata mitaani askari walitumia nguvu za ziada na vitisho vya hapa na pale kufungua njia ingawa bado walikuwa wabishi. Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema; "Wametufanyia mambo mabaya sana, hizi ni hujuma ambazo hazivumiliki, ndiyo maana nasema Simba haitakanyaga milele Kinshasa. "Hatutakuja kucheza mechi yoyote hapa kwa vurugu hizi, tutagawa pointi za bure. Labda Serikali itoe tamko na tupewe ulinzi maalumu au tucheze nje ya hapa. Na tutakwenda kushtaki Wizara ya Mambo ya Nje kuhusu unyama tuliofanyiwa hapa Kinshasa. "Tungeshinda tusingetoka hapa uwanjani, wangetuua hawa," alisisitiza kiongozi huyo, ambaye amependekeza ianzishwe vita dhidi ya raia wote wa DR Congo wanaoishi nchini kinyume cha sheria. Simba iliwasili jijini Dar es Salaam jana Jumatatu, saa 12.45 jioni kwa ndege ya KQ.[/TD][/TR][/TABLE]NOte: vita anayomaanisha hapa ni kuwakamata wakongo wanaoishi kinyume na sheria.wazamiaji
   
 2. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Naunga mkono hoja...............
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,515
  Likes Received: 19,937
  Trophy Points: 280
  Watanzania tuna mambo ya ajabu sana ambayo inabdi yakemewe kwa nguvu zote. tuna mtindo wa kuwahusudu sana wageni wakati ukienda kwao wewe wanakudharau na kukuona kuwa wewe si lolote si chochote. kuanzia kwenye ajira hatupendi kuweka uzalendo mbele ,wakongo wamejazana humu nchini na sisis tunawahusudu na kuwapigia makofi kila siku na dada zetu wakiwa mstari wa mbele kutoka na hawa wapata wanja wanaojichubua...tusipopendana wenyewe na kulindana hatutafika mabali.(ukiondoa ushabiki wa mpira)
   
 4. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kuna wanaotoka DR Congo kuja kwetu, eti ni ma expert wa kupamba maharusi...kana kwamba sisi hatuwezi kazi hiyo!!
   
 5. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,992
  Likes Received: 3,742
  Trophy Points: 280
  huu kweli si usanii uleule, wa siku zote na wa aina ileile wa maha-RAGE ya "gamba party"??

  maana maha-RAGE kwa visingizio........
   
 6. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Mwenzenu anatwatuliza munkari kiaina baada kuchezea kichapo kwa DCMP.Msanii huyo msimwamini sana anajua sana kuupepeta mdomo uwanjani zero.Muungwana ukifungwa unatia akili na mbinu zingine za kujipanga.VIPI RUFAA SAFARI HII HAINA MASHIKO?
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Si wakate rufaa CAF.......hahahaaaa
   
 8. 0717436862

  0717436862 Member

  #8
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama vp naye ajivue gamba2 tatizo rage maneno mengi alf hakuna ki2 apunguze usanii bwana! Aya akate rufaa tena!
   
 9. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  tukianzisha vita na wakongo ikiisha tugeukie Wasomali pia! Hivi huyu Rage ataweza kweli Ubunge na Uenyekiti wa simba!??? Time for excuses is no more!!
   
 10. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mimi najiluliza, hao washabiki ni wa DCMP au ni wale TP Mazembe wakitaka kulipa kisasi kwa fitna ya Simba?
  Tufanye TP Mazembe ndiyo Simba, wale fans wao wangefanyaje?
   
 11. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,281
  Likes Received: 4,286
  Trophy Points: 280
  Rage nae anachemsha sasa ,tuanzishe vita na DRC tutapigwa hawa jamaa wamezoea vita .Vita dhidi ya Uganda hadi leo imetugharimu halafu uanzishe vita na DRC.Vurugu katika soka hasa barani Africa ni kawaida unakumbuka ugomvi ya Misri na Tunisia
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,515
  Likes Received: 19,937
  Trophy Points: 280
  NOte: vita anayomaanisha hapa ni kuwakamata wakongo wanaoishi kinyume na sheria.wazamiaji
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Sishangai.....kumbe kasema Rage!
   
 14. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #14
  Jun 23, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni elimu yake haipishani sana na profesa maji marefu.
   
 15. x

  xman Senior Member

  #15
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  rage hasira hazifai, hivi sikuzote ukujua kama mpira wa kiafrika fitna muhimu, nawewe subiria wakija uku miaka ijayo mjipange tena
   
Loading...