Kuna vitu alivyofanya Makonda vikanishangaza kwanza sakata la WARIOBA, pili sakata la kuvamia kituo cha CLOUDS, tatu sakata la vyeti vyake na jinsi alivyofuatilia sakata la madawa vya kulevya. Pamoja na kuwa na marafiki na maadui wengi ila kwa kipindi hiki cha uongozi huu mtu ,taasisi au shughuri yeyote upende usipende ikifanywa kwa Baraka ya huyu mkuu wa mkoa itafanikiwa.Anajua mwenyewe mbinu anazofanya ila hata kwa Dar makonda anafanya kazi za waziri wa ulinzi, mambo ya ndani, Utamaduni, Elimu nk. Nakubaliana na mada MAKONDA akipewa DODOMA ataikimbiza sana na ukizingatia bado ana kazi ya kujipambanua vizuri mbele ya macho ya watu kwani madoa ya Dar es alaam bado yapo na pasingekuwa na yale madoa katika utendaji wake huko nyuma pale Dar basi MAKONDA angekuwa ni mwanasiasa aliyefanikiwa kwa muda mfupi katika kipindi hiki cha awamu ya tano.MAKONDA APELEKWE DODOMA akatengeneze jiji.Dar ilishaharibika sana waachiwe wazee