Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,174
- 17,635
Zaidi ya vijana 1,000 wa Mkoa wa Arusha, leo Machi 26, 2025 wamefika katika ofisi za mkuu wa mkoa huo kwa ajili ya kufanya usaili wa kuwania nafasi za ufadhili wa masomo nchini India.
Vijana hao wamejitokeza kufuatia tangazo la Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kuwa Serikali ya India imetoa ufadhili wa masomo kwa vijana 1,000 wa Arusha.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa usaili huo, Makonda amesema ufadhili huo utahusisha programu na fani zaidi ya 250, na unasimamiwa na Serikali ya India kupitia kwa Balozi wake nchini Bishwadip Dey.
Soma, Pia: Makonda awatafutia vijana nafasi 1000 za kusoma nchini lndia. Huyu kijana ni kiongozi mbunifu sana, Rais Samia mtumie vizuri Makonda
Makonda amesema fursa hiyo imetokana na juhudi kubwa alizozifanya Rais Samia Suluhu Hassan za kuimarisha uhusiano mzuri na mataifa mbalimbali, juhudi zilizozishawishi nchi kama India kutoa fursa hizo za masomo kwa vijana wa Kitanzania.
"Hii ni fursa adhimu kwa vijana wa Arusha kupata elimu bora nje ya nchi hususani nchini India ambayo inajulikana kwa ubora wa elimu yake katika nyanja mbalimbali," amesema Makonda
Soma: Kuelekea Uchaguzi 2025: Vijana tunafanya nini kuongeza ushiriki wenye tija na kuwapata viongozi bora wasioendekeza uchawa?
Kwa upande wao baadhi ya vijana waliojitokeza wamesena usaili huo ni hatua kubwa kwao katika kufikia malengo yao ya kielimu na kimaendeleo.