window phone 8 hiyo itakua kama picha inavoonesha
Kuna vitu vipya ambavyo wp8 wamejitahidi kueka ambavo kwenye ios na android hawajafkiria kua navyo
arched keyboard
Tupo wengi tunakula kucha simu za touch inakua ngumu kupatia button mara kibao tunakosea wp8 wametuskia keyboard kama ya simu za zamani kwenye touch screen hata kama una mdole gumba mpana kama muhuri wa tanesco utachat vizuri tena kwa
mkono mmoja
Kama unavoona qwe unatouch sehemu 1 na sio 3 tofauti.
maps
wote tunajua maps za nokia ni better kuliko google maps linapokuja swala la coverage kwenye wp8 kutakua na nokia maps na kizuri zaidi unaweza fanya offline maps kwa kudownload eneo fulani kwa ajili ya matumizi ya badae
Mfano kesho nataka niende kijijini kwetu
sigimbi na hakuna internet au ipo ya slow yani edge tu na nataka ntumie ramani ntaidownload yote ramani ya sigimbi and then kesho nkienda ntatumia bila internet
child friendly os
Watoto wazee wa chabo imekula kwenu hii os itakua na parental control ambayo itablock vitu ambavyo owner hataki mwanae avione
right to left language support
Jamani si lugha zote zinaanzia kushoto kuelekea kulia lugha nyengine kama kiarabu kinaanzia kulia na kuenda kushoto wp8 wamead hii feature kuwavutia zaidi wateja wa midlle east.
bluetooth
Tushazoea bluetooth kukonekt na device kama earphone na kuhamisha mafile ila kwa wp8 bluetooth ina mambo mengi sana ikiwemo peer to peer (p2p) yani mtu mbili zitashare files na folder kama ni device 1. Wewe unaweza niruhusu mimi uhuru wa folder lako fulani ie, music then nachagua mwenyewe nyimbo ya kujirushia.
Pia wame advance kwenye app na device zengine.
new start screen
Kama ilivo wp7 screen ina vitiles tiles kama vibox box hivi, windows phone 8 itakua navo pia lakini hivi vitakua vya ukweli maana utavieka the way unavotaka mfano application unaipenda basi icon yake utaifanya ionekane kubwa kwenye screen
internet explorer 10
Hii ndo itakua default browser na kama unavojua ie10 itakua html5 supported so mambo ya kueka flash ili uangalie youtube yataisha.
Tena ina browser security website zenye virusi na mbovu zitakua detected na utaulizwa kama unataka kuingia au hutaki
x-box
Ninaposema xbox watu wote wanaopenda magame washalijua ni competitor wa ps3 sasa atakua ndani ya simu yako ni wewe na mda wako tu.
enterprise ready os
wp8 ina tons za advance technology kwa ajili ya it admin ili waweze kuwamanage employees tutegemee hizi simu kusambaa makazini kwa sababu boss atawamonitor kwa simu hizi (intranet)
- hapa hapa kuna company hub ambayo microsoft tayari wanaitumia ofisin kwao maswala ya kuomba ruhusa kumuona bosi kila kitu ni simu hizi
camera
Hapa kuna vitu viwili vikubwa
-self timer utege mda kabla camera kujipiga
-smart group photo shoot yani mfano mnapiga picha watu wa 4 ila kuna mhusika mmoja mkubwa basi utaidirect camera then atatoka vizur kuliko wengine
in application purchase
Application utainunua humo humo ndani ya app hii itazuia wizi na uchakachuaji hence itawavutia developers
tujiulize sasa
Je window phone 8 ni android na ios killer? Android wao kimya ios ye atazindua iphone 5 wiki baada ya nokia world je iphone naye atajibu mapigo kwa ios 6?
muhimu: blogers wa kibongo mjifunze kuandika post zenu na muache copy an paste za jf