I need a born again husband

je unafahamuya kuwa ndoa ni agizo la Mungu?
kama una huo ufahamu tafakari yafuatayo
i/ kama vile ilivyo kuwa mke mwema mtu hupewa na Mungu vivyo hivyo mume mwema mtu hupewa na Mungu.
ii/ tunatambua ya kwamba mtu aliyeokoka na ana mahusiamo mazuri na Mungu kupitia Yesu Kristo huwa anafahamishwa juu ya mambo yajayo ikiwa ni pamoja na mke/mume mwema, je aliyekuelekeza uje jf kujitafutia mume ni Mungu au hulka zako kwa sababu unataka kuolewa?
iii/ Mungu hampi kitu mtu kwa sababu ameomba ila kwa sababu ni sawa na mapenzi yake, una uhakika gani hivyo vigezo vyako ulivyoviweka ni sawa na mapenzi ya Mungu na sio hisia zako?
fikiria hizi hoja chache kwa umakini maana sitamani sisi tuliokoka tenende kama watu wasiomjua Kristo.
 
kwa hiyo wachagga hawjaokoka?
nyie ndo wale wale waliosema hakuna kitu chema chaweza tokea nazareti.
tambua ya kwamba kabla injili ya Yesu Kristo kuja Africa babu zetu walikuwa wanaabudu wasichokijua na kazi ya mikono yao(sanamu) lakini baada ya KWELI(Neno) kuhubiriwa kwa wazee wetu wa wakati huo waliikubali na kuiamini injili, wakaziacha njia zao mbaya na ibada ya kuabudu kisicho Mungu. na napenda nikutaarifu kama kuna eneo ambalo injili ilipokelewa bila upinzani mkubwa ni eneo la kilimanjaro na kama huaamini jaribu kufuatilia vizuri.na swala la kuwa wachagga wakiokoka hawaachi mila zao hilo sikubaliani nawe hata kidogo, inaelekea aliyekueleza jambo hili hajuia alichokuambia, ukiifahamu kweli, kweli itakuweka huru na haitakupa shida kushirikiana na mchaga kwani biblia inasema mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom