I gat this serious problem!

I gat this serious problem!

I had the same problem before ila namshukuru Mungu limeisha. Ushauri wangu kwako.
  • Punguza matumizi yako binafsi (si umesema huna familia?) kama ulikuwa unakunywa acha au kama huwezi punguza walau kunywa weekend tu. Jenga tabia ya kununua mahitaji yako ya jumla ya mwezi.
  • fungua fixed bank account, kila mwezi unaweka kiasi cha pesa hata laki 2 tu, inatosha.
  • Hatukatai kusaidia ndugu/wazazi na jamaa ni wajibu wako lakini saidia kwa mpango! SIo kila mwezi wewe wakutumia watu pesa. Kama wewe ndie mtegemezi mkuu ktk familia yenu, wataftie wazazi walau biashara iwasaidie kujikimu badala ya kukutegemea wewe kwa 100%
  • Epuka sana madeni ndugu yangu na uyakatae kabisa!!Kopa kwa lengo maalum la kimaendeleo. I mean unakopa labda unafungua biashara ambayo mwisho wa siku inakupa faida. Epuka kukopa ili umpe mtu msaada au kwa ajili ya kunywa bia.
MWISHO jifunze UBAHILI na UKAUZU! Mimi siku hizi ni kauzu zaidi ya dagaa!Nikimsaidia mtu namsaidia ule msaada unaohitajika not otherwise. Ukifanya hivyo utaweza kujiwekea akiba na kufanya shughuli za maendeleo. Jipange ndugu wakati bado uko single ukioa na hali hii walaahi utafanyiwa mbaya

Daaaah sante sana mkuuu....such a convincing advice...thanx much much....
 
Fanya hivi nunua mahitaji ya mwezi Mzima hasa chakula...halafu panga kiwango cha matumizi ya vitu kama simu kwa mwezi iweje...acha nunua maji ya chupa...nunua ya lita 10 na kuendelea

ACHEMSHE MAJI YA KUNYWA TU!! Anunue birika lile la umeme then amemaliza. Before nilikuwa nanunua maji ila siku nilipoyapanga yale madumu ya maji (kipindi hicho yanauzwa 1,000) nilitamani kulia. NImeapata sitonunua maji ya kunywa kwa matumizi ya nyumbani kamwe (labda ya mtoto mchanga tu, akikua mwendo mdundo)
 
No usikate Tamaa
Kama una girlfriend muweke jirani nawewe at list ata Ku control hususani kwenye mshahara wako

Inategema ana girlfriend wa aina gani. Hawa wa siku hizi wa kidigitali aisee itakula kwake.
 
Asee girlfriend tena aje ku control mshahara!!

Ndio wapo ambao wanajuwa how life is going on
Nasio wote michaluko and sometimes mwanamke anaweza akawa mshauri mkuu katika maendeleo
 
Kama upo serious na unamaanisha unachokisema,gawa hiyo pesa yako mara tatu,theluthi moja weka benki na ATM mkabidhi mama mzazi kama yuko mbali nawe,theluthi nyingne ipangie matumizi yako ya kawaida,na theluthi ya mwisho ndo iwe ya ndugu,starehe na mengineyo.
Fuata huu utaratibu wakati ukitafta namna ya kuwekeza,inaonekana matumizi yako ni makubwa kuliko mapato,hivyo ni lazima uongeze njia zako za kujiingia kipato.YOU CAN THIS OR YOU CAN LIV THIS,THE CHOICE IS YOURS!.
 
kama unatumia pombe acha. na wanawake punguza. usimuibie Mungu namaanisha toa 10 percent kuepuka mifuko kutoboka . pia jijengee kuwa na displine na fedha inayo pita mikononi mwako.
 
By nature hawa watu ni watunzaji wazuri sana wa pesa, wanajua maisha acha kbs

Nilikua silijui hili mkuu,naelewa unaweza ukaoa ukapata nuksi kiuchumi maishani ama ukapata baraka kiuchumi,unataka kusema hayo makabila ndo waleta baraka kiuchumi ndoani?
 
Nilikua silijui hili mkuu,naelewa unaweza ukaoa ukapata nuksi kiuchumi maishani ama ukapata baraka kiuchumi,unataka kusema hayo makabila ndo waleta baraka kiuchumi ndoani?

huwezi kuwavunajua vitu vyote duniani so usijishangae kutojua. Nuksi au baraka mi sijui ila ukitaka hela ikae oa hayo makabila kingaz n chaggaz(machame), nenda K/koo ndio wenye premises za nguvu na biashara kubwa

Sent from my iPad using JamiiForums
 
ok mkuu let me take it as a challenge,nafikiri mleta mada atakua amekusoma nae pia japo nabaki na lakini lakin nyingi
 
Fanya hivi nunua mahitaji ya mwezi Mzima hasa chakula...halafu panga kiwango cha matumizi ya vitu kama simu kwa mwezi iweje...acha nunua maji ya chupa...nunua ya lita 10 na kuendelea

Nimeipenda sana hii. Nami namshauri ivo ivo
 
Fanya hivi nunua mahitaji ya mwezi Mzima hasa chakula...halafu panga kiwango cha matumizi ya vitu kama simu kwa mwezi iweje...acha nunua maji ya chupa...nunua ya lita 10 na kuendelea

Asante "the boss" kwa ushauri mzuri....by tht i can surely improve somthn..
 
tafuta biasahara ufanye

pia punguza idadi ya unaowapa fedha, yaani inakuaje unakopa ili umpe mtu hela? kama mlengwa haumwi ?
 
By nature hawa watu ni watunzaji wazuri sana wa pesa, wanajua maisha acha kbs

Nimekumbuka chuo i had this gal aliwah kuniambia kwa namna nnavyojiaxhia na maisha km cntampata gal mwenye akil kuni-control i wil die poor....now i see coz she knew me for almost 2 yrs means she knows alot.....
Alikuja akigoma mara nying mm kuwasaidia watu...she said like bado haujawa na uwezo wa kutoa msaada..i thout ana roho mbaya bt now i c wat she meant
 
Kwanza, hii inategemea na umri wako, muda uliokuwa kazini na mengine.
Wakati naanza kazi nilikuwa na tatizo kama lako, mbaya zaidi mie kazini nilikuwa napata kila kitu, kuanzia chakula hadi vocha ya simu, na bia juu free.

Lakini nilikuwa najikuta hadi nimeomba advance ya mshahara kwa shida zisizo zangu kwa kama miezi 7 ya mwanzo. Kuna siku dada mmoja alisema mno tabia ya advance, yale maneno yaliniingia, nikaapa kutochukua.

Sasa ikabaki mwisho wa mwezi, uwiii nakutana na mambo meengi, hela yote kwishney. Nikahamia sehemu tofauti, majukumu yangu binafsi yakaanza kuongezeka maana sehemu nilohamia hakukuwa na huduma kama za awali, basi nikaanza kujipanga taratibu na kuanza kuwa mchoyo a bit.

Baada ya muda nikaona nafanya kazi, lakini nipo nipo tu. Nikaanza kujipangia malengo ya muda mrefu na muda mfupi. Labda unapanga, baada ya miaka miwili nataka niwe na hiki, unapanga kulingana na kipato chako. Una unajaribu kujistretch to your limits, ili hata usipofika ulipopanga uwe umefika mahali fulani.

Kama wewe naweza kupangia hiki, kabla mwaka haujaisha, walau uwe na kiwanja, hata kama itakubidi kulipa taratibu. Najua kwa logistic za Dar baadhi huanza na magari, hii itategemea sana kipato chako, usije ukanunua halafu pesa ya kulihudumia daily likakwamisha mambo yako mengine.

Kama bado unaishi kwenu, jipe azimio la kuhama na kupanga chumba chako, nunua vitu vya ndani unavyohitaji, kidogo kidogo unaanza kujifunza nidhamu ya pesa.

Kutunza pesa ni kitu unajifunza, hakiji tu, unajifunza taratibu. Ina maana gani wewe kufanya kazi halafu maisha yako yako vile vile kila siku? Elimu yako itakuwa haijakukomboa. Kama umeshagundua hili, jua uko kwenye direction sahihi kabisa.
 
I had the same problem before ila namshukuru Mungu limeisha. Ushauri wangu kwako.
  • Punguza matumizi yako binafsi (si umesema huna familia?) kama ulikuwa unakunywa acha au kama huwezi punguza walau kunywa weekend tu. Jenga tabia ya kununua mahitaji yako ya jumla ya mwezi.
  • fungua fixed bank account, kila mwezi unaweka kiasi cha pesa hata laki 2 tu, inatosha.
  • Hatukatai kusaidia ndugu/wazazi na jamaa ni wajibu wako lakini saidia kwa mpango! SIo kila mwezi wewe wakutumia watu pesa. Kama wewe ndie mtegemezi mkuu ktk familia yenu, wataftie wazazi walau biashara iwasaidie kujikimu badala ya kukutegemea wewe kwa 100%
  • Epuka sana madeni ndugu yangu na uyakatae kabisa!!Kopa kwa lengo maalum la kimaendeleo. I mean unakopa labda unafungua biashara ambayo mwisho wa siku inakupa faida. Epuka kukopa ili umpe mtu msaada au kwa ajili ya kunywa bia.
MWISHO jifunze UBAHILI na UKAUZU! Mimi siku hizi ni kauzu zaidi ya dagaa!Nikimsaidia mtu namsaidia ule msaada unaohitajika not otherwise. Ukifanya hivyo utaweza kujiwekea akiba na kufanya shughuli za maendeleo. Jipange ndugu wakati bado uko single ukioa na hali hii walaahi utafanyiwa mbaya

Thanx alot mkuuu...thanx alot kwa ushaur mzuri
 
una miaka mingapi kazini? Nafikiri kabla ya ushauri tuanzie hapo kwanza
 
Back
Top Bottom