I am single again

Tuttyfruity

JF-Expert Member
Dec 3, 2017
2,266
2,000
Nianze kwa kusema hili sio tangazo. Siwezi nikajitongozesha JF.

Anyways tuende direct kwenye mada. I am newly single guys. Hakuna kitu nachukia kama kuwa single ila ndo ishakuwa nifanyeje.

Huyu chalii nilikutana nae few months ago yani alikuwa na kila kitu nilichokuwa natafuta. Nikajiona nimefika bhna, kumbe! .

Ukistaajabu ya musa utayaona ya Firaun hakukosea kabisa. Huyu chalii kilichonishinda yani marafiki zake anawanyenyekea sijui kama kitu gani. Yani tunaweza kuwa kitandani ila rafiki yake yeyote akimpigia simu akamchukue mahali ataacha kila kitu akamchukue yani inshort kama anawehuka fulani hivi.

Ana ratiba zake Jumamosi jioni lazima akawanunulie washkaji zake pombe walewe Jumapili anajaza gari mafuta wanaenda kula bata. Anawafuga nyumbani kwake chakula pombe kila kitu juu yake. Yani nimestaajabu sana. Sijawahi kukutana na zahma kama hii.

Imefika wakati nikawaza labda jamaa shoga coz it doesn't make sense. Mtu unawapapatikiaje na kuwaogopa wanaume wenzako hivi. Siku asipopokea simu zao wananuna na yeye anakosa raha.

Yote tisa muda na mimi hana kabisa. Bora hata angekuwa na wanawake wengine ningejua cha kufanya. Wanaume nitashindana nao vipi mimi

Mwanzo ilikuwa tukitoka on a date lazima aje na jamaa yake nikampiga stop. Nilimwambia kama huwezi kuja peke yako its better usije kabisa. Si akaacha kutoka na mimi 😂😂😂 nikaona hapa hamna mtu hapa.

Anyways aluta continua! Mapambano lazima yaendelee. Dua zenu wadau.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom