Huyu si Lowassa ambaye UKAWA tulimtaka

Huyu si Lowassa ambaye UKAWA tulimtaka

Chrisludos

Senior Member
Joined
Oct 12, 2012
Posts
135
Reaction score
41
Lowassa ambaye wengi wetu tulimtaka ahamie UKAWA, si huyu ambaye tunamshuhudia.

Kutaka kunielewa zaidi, hebu jaribu kukumbuka mkutano wake wakati wa kutangaza nia pale Arusha na ufananishe na mkutano wake wa leo Arusha.

Mkutano ule wa kwanza, ulionyesha kujiandaa.. Wasanii walijaa, vyombo karibu vyote vya habari vilikuwa live..

Tatizo sasa hivi liko wapi? Hana hela au ameishiwa? Bado sana kujihakikishia ushindi, tunahitaji kuongeza nguvu ktk media, na pia kama inawezekana kuweka wasanii pia si vibaya kwani lengo ni kumpata kila mtu.

Hebu pata picha mikutano ya UKAWA inavyojaa leo bila wasanii wakubwa, je wangekuwepo ingekuwaje? Wengine watabisha kwa hoja dhaifu ya kujitofautisha na CCM, bila kusahau lengo letu kubwa ni kuingia madarakani ndo maana tukamfanya Lowassa kuwa mgombea wetu.

Muda bado ungalipo, tubadilike.
 
Pamoja na hayo yooote TANESCO Fisiemu wasinge tuachia Umeme
 
Pamoja na hayo yooote TANESCO Fisiemu wasinge tuachia Umeme

Wasingeweza kukata nchi nzima, pia kumbuka si wote wanatumia umeme wa TANESCO.. Na tunataka mikutano yote iliyobakia iwe live.
 
Zimebaki siku 17= two weeks
 
Mbona huijui Chadema sasa, ww ni gamba

Kuijuaje? Acha kukariri kilaza wewe, nyakati zinabadilika.. Kuna watu hawana hobby ya siasa but wanapenda mziki kwakuwa tunahitaji kura zao si mbaya kuwawekea wasanii.
Na kuhusu matangazo kuruka live, kumbuka si wote wana nafasi ya kufika katika mikutano... Tvs na radios zinawezesha kifikia wananchi wengi zaidi.
 
Kuijuaje? Acha kukariri kilaza wewe, nyakati zinabadilika.. Kuna watu hawana hobby ya siasa but wanapenda mziki kwakuwa tunahitaji kura zao si mbaya kuwawekea wasanii.
Na kuhusu matangazo kuruka live, kumbuka si wote wana nafasi ya kufika katika mikutano... Tvs na radios zinawezesha kifikia wananchi wengi zaidi.
wewe ndio kilaza gamba, unajua efforts zilizofanywa na hujuma zilizofanywa ili matangazo yasiruke live.

Wasanii walionunuliwa utawapata wapi, sio kila msanii anaweza kuvuta watu.
 
Huenda Lowassa akawa amebadilika kwa mtazamo wako, ilimradi CCM tunayotaka kuiondoa ni ileile, ntaendelea na maamuzi yangu ya kumchagua October 25!
 
Huenda Lowassa akawa amebadilika kwa mtazamo wako, ilimradi CCM tunayotaka kuiondoa ni ileile, ntaendelea na maamuzi yangu ya kumchagua October 25!

Nafurahi kama utampigia kura, vipi na wale ambao bado hawajafanya maamuzi? Tunawapataje?
 
Nafurahi kama utampigia kura, vipi na wale ambao bado hawajafanya maamuzi?
Tunawapataje?

Natambua na kuelewa umuhimu wa unachokisema na kukisisitiza hapa, kumbuka kwamba kuna juhudi na hila nyingi sana zinazofanywa kukwamisha kila mbinu za kampeni za ukawa kwa uchache, kutumika kwa aliyekua katibu wa cdm, wasanii waliokua cdm kununuliwa, kuandaliwa kwa wanachama feki wa cdm waonekane wamefanya fujo na kukamatwa n.k hata kwa hili la kurusha mikutano hewani moja kwa moja limegubikwa na ukakasi huo huo mkuu.

Cha kufurahisha ni kwamba, ccm imewafikisha wananchi walio wengi mijini na vijijini kutamani na kuhitaji mabadiliko.
Watu walishaamua na wameamua nani watampigia kura tangu wakati wanajiandikisha zoezi la BVR, siasa zetu zingekua zinategemea sana sera na kampeni, CCM isingekua madarakani hadi leo hii, tungeisha isahau kitambo sana.

Wakati mwingine sio vizuri kupoteza rasilimali pale unapofahamu hapatakua na matokeo bora ya uwekezaji, kwa hali ya umeme na hila zinazoendelea, isingekua na tija sana kupoteza pesa kwa huu mkutano mkuu. Haya ni maoni yangu!
 
mabadiliko ya kinyonga kubadilika rangi hayamtoi kwenye kundi la vinyonga

Kinyonga anabadilika kuakisi kile anachokiona/mazingira aliyeko....anaweza akawa wa blue kama yuko kwenye maeneo ya blue na anaweza kua mwekundu kama yupo kwenye eneo la rangi nyekundu, kipi ni kikgumu kinyonga kubadilika au mazingira kubadilika?
 
Back
Top Bottom