Wenzako wabishi sana. Ukiwakosoa wanakuita gamba. Ubishi huu ndio unawapeleka kaburini. Watazikwa wazima wazima safari hii.jadili hoja, mi ni CHADEMA kabla we hujaanza kufatilia siasa.
Kinyonga anabadilika kuakisi kile anachokiona/mazingira aliyeko....anaweza akawa wa blue kama yuko kwenye maeneo ya blue na anaweza kua mwekundu kama yupo kwenye eneo la rangi nyekundu, kipi ni kikgumu kinyonga kubadilika au mazingira kubadilika?
Upo sawa ni vigumu kwa mazingira kubadilika. je kinyonga anapobadilika rangi na kuwa wa blue kwa kufuata mazingira ya blue kunamfanya abadilike na tabia yake aliyokua nayo alipokuwa kwenye mazingira ya rangi nyekundu?
Hapo nikuachie wewe ulieleta mfano wa kinyonga kwenye suala la rais. Mimi kazi yangu ilikua kujibu kwa mujibu wa bandiko lako.
Sasa hivi tunataka tupake rangi nyekundu kua ya blue, hatuhangaiki na kinyonga atafuata rangi ya mazingira aliyopo.
Sasa wee ushakubali mikutano ya ukawa inajaa haswa bila wasanii...unawataka wa nini ilihali mikutano inajaa? Pili, sio mpango kuwaleta watu wafate wasanii. Watu wanatakiwa wavutwe na lengo kuu ambalo ni kusikiliza wagombea, sio wasanii
Aya mkuu tusubiri oktoba 25
Lowassa ambaye wengi wetu tulimtaka ahamie UKAWA, si huyu ambaye tunamshuhudia.
Kutaka kunielewa zaidi, hebu jaribu kukumbuka mkutano wake wakati wa kutangaza nia pale Arusha na ufananishe na mkutano wake wa leo Arusha.
Mkutano ule wa kwanza, ulionyesha kujiandaa.. Wasanii walijaa, vyombo karibu vyote vya habari vilikuwa live..
Tatizo sasa hivi liko wapi? Hana hela au ameishiwa? Bado sana kujihakikishia ushindi, tunahitaji kuongeza nguvu ktk medias, na pia kama inawezekana kuweka wasanii pia si vibaya kwani lengo ni kumpata kila mtu.
Hebu pata picha mikutano ya UKAWA inavyojaa leo bila wasanii wakubwa, je wangekuwepo ingekuwaje?
Wengine watabisha kwa hoja dhaifu ya kujitofautisha na fisiemu, bila kusahau lengo letu kubwa ni kuingia madarakani ndo maana tukamfanya Lowassa kuwa mgombea wetu.
Muda bado ungalipo, tubadilike.
we Ni mrundi? hujui kuna
Hujuma rushwa, dhidi ya upinzani? uwanja wa mapamban hauko sawa
Ndugu hujui huyo ni gamba amebadili ID yake kaja na mpya? Soma vizuri Jina lake.
mabadiliko ya kinyonga kubadilika rangi hayamtoi kwenye kundi la vinyonga