Huyu Pogba wetu ni hasara tu

Huyu Pogba wetu ni hasara tu

Lituye

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
1,864
Reaction score
5,697
Wanajamvi mtakumbuka wakati wa usajili tuliambiwa hii timu yetu sasa inasajili bonge la fowadi anayekuja kumaliza matatizo yote.

Hata kuingia kwake ktk timu alikuja na mbwembwe kibao, Mara kufanya mazoezi ya ghafla klabuni usiku au mchana akiwa na waandishi Wa habari ili mradi ajioneshe tuu kwa mashabiki kuwa anauwezo.

Cha kushangaza ligi ilipoanza ameanza kuja na Masharti kibao klabuni eti ili aonekane kuwa yeye ni mchezaji mzuri kuliko Wa timu pinzani tumtimizie mambo yafuatayo.

1. Mabeki wa timu pinzani wote wafungwe miguu na mikono wawapo uwanjani.

2. Timu yetu iwe inapewa penati kila mechi na marefa ili yeye awe mfungaji bora.

3. Timu pinzani zisiruhusiwe kuleta mashabiki uwanjani.

Sasa wenye Akili hapa klabuni tukaanza kuhoji huyu kweli ni fowadi au garasa?
Mbona fowadi tuliye muacha alikuwa anafunga magoli huku mabeki Wa timu pinzani wakicheza japo tulimuona kama kashuka kiwango?

Tena timu pinzani ziliruhusiwa kwenda kwa ndege helcopta au usafiri wowote kokote hapa nchini kuchukua mashabiki na kuwaleta uwanjani katika mashindano mbali mbali.

Uchumi Wa klabu umeshuka ghafla mashabiki hawana imani naye tena kabisa. Wanajiuliza fowadi gani hawezi cheza mechi za kimataifa anag'ang'ania mechi za mchangani tuu.

Huyu Pogba klabu imepata hasara kubwa Sana kwa kusajili mchezaji bila hata kuangalia uzoefu na historia yake hapa klabuni. Anazua hofu ubabe na kushabikia magoli ya mikono eti yawe halali kwa timu yake tuu.
 
ah pogbaaaaaa...
pogba nasikia amekuwa mnyang'anyi mtaani,eti mali za washabiki wake zote zinapaswa azimiliki yeye...
na ukitaka kumjua pogba vizuri mwambie hujui kucheza mpira...
hapo mechi utazisikia ukiwa gerezani...
pogbaaaaaaaaaaaaa...
akijibu hoja jiandae kushangaa kwamba ni msomi au kila.za wa mpira.
 
Makala fupi nzuri na yakufikirisha zaidi,tujiulize sisi mashabiki ni nani alimsajili pogba?ni shilling ngapi zilitumika? Na je tunauzoefu na usajili wa dirisha dogo?mana huyu kasajiliwa dirisha dogo masaa machache kabla usajili kufungwa !!!
 
HAMNA POGBA YUKO FRESH TU SEMA WABONGO TUNABEBEWA SANA AKILI ZETU NA TUNATUMIKA KWA KUDANGANYWA NA MAKOCHA WA TIMU PINZANI KAMA HATUKO TIMAMU. KWA KIFUPI MAKOCHA NA VIONGOZI WA TIMU PINZANI WAMESHINDWA KUFUNDISHA NA KUENDESHA SOKA LA UKWELI,WAMEBAKI KUFANYA POROJO TU WANAPOKUWA HUKO CNN,SKY NEWS,BBC NK! ILA POGBA KIWANGO BADO KIPO CHA KUELEWEKA TU. HALAFU YATUPASA TUMPE JAPO HATA MIAKA MIWILI HUYU POGBA!!
 
Makala fupi nzuri na yakufikirisha zaidi,tujiulize sisi mashabiki ni nani alimsajili pogba?ni shilling ngapi zilitumika? Na je tunauzoefu na usajili wa dirisha dogo?mana huyu kasajiliwa dirisha dogo masaa machache kabla usajili kufungwa !!!
Tungefanya Usajiri,ila Pesa Hamuna Si Unajua Timu Imepata Hasara Baada ya Hisa Timu Kushuka!Matokeo Mabovu ya Mfululizo Yamewakimbiza Wengi!Labda Tusubiri Mkataba Wake Utakapo Expire 2020!Labda Twaweza Mwachia Aende!
 
Back
Top Bottom