Huyu ni yule tuliyemsubiri au tuendelee kusubiri?

Agresive

JF-Expert Member
Feb 18, 2018
889
1,226
Nawasalimu kwa JMT.

Katika miaka 5 iliyopita hakuna rangi ambayo hatujaona.

Ni kipindi wafanyabiashara walihama nchi.

Kodi ilikusanywa kibabe na akaunti kufungwa.

Kesi za kubambikiziwa uhujumu uchumi zilitamalaki.

Wahitimu wa vyuo walisahau kabisa kuhusu ajira.

Watumishi waliambia sitaongeza mshahara wala kupanda daraja,

Tulilazimishwa kupiga makofi na vigelegele kwa jambo zuri au baya.

Wanasiasa wa upinzani waliota joto la jiwe.

Katika yote hayo mtendaji mkuu master akijiita mtetezi wa wanyonge, wakati wanyonge wakilala njaa na kuambiwa maneno kuwa barabara zinajengwa,ndege kununuliwa vitu vyote hivyo vinawahusu.

Mungu hana kamati akafanya maamuzi,magumu sana.

Awamu ya 6 ikaja na maneno mapya kabisa ya kutia moyo.

1. Sitaki kodi ya dhuluma

2. Vyombo vya habari vifunguliwe

3. Sitaki uongozi wa kunyanyasa watu isipokuwa haki itendeke.

4. Wafanyabiashara na wawekezaji watengenezewe mazingira rafiki.

5. Mahusiano mema na nchi jilani na jumuiya ya kimataifa.

NAENDELEA KUJIULIZA KATIKA YOTE HAYA JE

Huyu ndiyo tuliyemtarajia mkombozi wetu au tuendelee kusubiri!!!
 
BADO NAJIULIZA KWA NINI SHEKH KISHIKI HAWAMUHOJI KWA YALE MATAMSHI ALOTOA DHIDI YA MBANGI SELE??
 
Ni sahihi maisha ni yako na ukombozi ni wako lakini mfumo wa haki katika uongozi ndiyo msingi wa yote.

Akina Manji wamehama nchi je walikuwa hawajitafutii riziki na kulipa kodi???
unatetea majambazi!!!
 
BADO NAJIULIZA KWA NINI SHEKH KISHIKI HAWAMUHOJI KWA YALE MATAMSHI ALOTOA DHIDI YA MBANGI SELE??
Kwa sasa mambo yanaenda pole pole si,kama zamani mkuu.

Hata zamani shida sana ilikuwa ukimchafua Jiwe ndiyo ungetambua kuwa yeye ni nani.
 
Kiroho kabisa, huyu ndie kiasi tu, Bado kidogo hajae anakuja ni mda tu ,japo aliopo atajitahidi kidogo but mwenyewe haja sio huyu bali mwenyewe haja asema bwana
 
Back
Top Bottom