Huyu ni Wakili 'wa kutegemewa' na si wakujitegemea

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Ni Wakili Mwandamizi pale Tanganyika Law Society (TLS). Ni Wakili mbobevu lakini kwa ndani ni 'mwonevu'. Kutokana na ukongwe na ubobevu wake, TLS na hata 'wanaharakati' huwa hawamkosi kwenye majopo yao ya Mlalamikaji au Walalamikaji.

Ni mjenzi mzuri wa hoja za haja. Ana Kampuni yake ya Mawakili. Lakini, si Wakili wa Kujitegemea tu; ni Wakili wa Kutegemewa na Serikali. Huingia kupoza mambo. Huingia kujenga hoja tulivu na zinazopunguza maumivu bila kutia uvivu lakini lengo hutimia.

Miaka zaidi ya 20 uwakilini. Hakosekani kuanzia Dar es Salaam hadi kule Mbeya kwenye majopo ya Mawakili wa Walalamikaji dhidi ya Serikali. Kwakuwa TLS pia wamejaa 'wa Serikali', huwa rahisi kwake kupenya na kuteka majopo. Akishakuwa kinara kama mnara, hi=uifanya kazi yake vyema.

Wakili mbobevu, mkomavu, mzoefu asiye mrefu lakini maarufu sana. Wakili wa kupigiwa mfano. Huweka mambo sawa na hukaa pembeni kwa amani akisubiri 'dili' lingine. Kule kwetu kwa wakati ule huita 'kuteka kijiji kwa ajili ya kulifurahisha jiji'.

Anaichapa kazi yake kwa weledi mkubwa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Nachingwea, Lindi)
 
Back
Top Bottom