Huyu Ni Mwizi Gani Jamani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu Ni Mwizi Gani Jamani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by PakaJimmy, Jul 30, 2009.

 1. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  TRUE SCENE!...Imetokea!!

  Nina jama yangu anayeishi na kufanya kazi Mbeya, ambaye kwa bahati mbaya aliibiwa simu yake katikati ya mwezi huu July 2009, akiwa kwenye Hiace!

  Huyu jamaa, kabla ya hapo, alikuwa ametuma maombi ya kufanya Matriculation Exam Arusha University.

  Katika hali isiyo ya kawaida, inaelekea mwizi wa simu yake siku moja aliweka chip iliyokuwa kwenye simu ya huyu ndugu yangu, na mara alipoweka alikutana na meseji iliyotumwa na Arusha University kuhusiana na tarehe ya Matriculation Exam!

  Mwizi huyo aliamua kuiforward meseji hiyo kwenye namba mbalimbali zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye hiyo line hiyo, na hatimaye ujumbe ukamfikia huyu ndugu yangu, ukieleza tarehe, mahali,eneo, na muda, ambapo ishu hiyo ingefanyika, ambapo ni jana(29/7/2009)!

  Huyu jamaangu alisafiri kwenda Arusha na KWELI KABISA ilikuwa ndo tarehe ya Exam hiyo, na amefanya, na leo 30/7/2009 yuko kwenye basi akielekea Dar na hatimaye Mbeya!

  Sasa sijui mwizi huyu awekwe kundi gani!
  Ni mtu mwenye huruma, au ni msomi, au mpumbavu au genius?
  Embu wanaJF nisaidieni kumchambua mtu wa jinsi hii!
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wezi nao ni binadamu, kuna wakati utu huchukua eneo lake. Hivyo huyo ni Mwizi lakini kiutu aliona kuwa yani kaiba simu, na pia amkoseshe jamaa Exam. Lakini pia huyo Mwizi kiasi fulani atakuwa kaenda shule, mpaka kajua ubora wa Elimu. Ila ni Mwizi.
   
 3. GP

  GP JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  wizi huu kidogo una akili kiasi chake, katumia ubinaadam!
   
 4. E

  Exaud Minja Member

  #4
  Jul 30, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 84
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Huyu ni mwizi tu si mchawi na shule ameenda pia, shida yake ilikuwa simu tu, huyu anaweza hata akakutumia chip yako akijuwa contact address yako.
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  He/she is an educated thief but a thief non the less. Haja mfanyia jamaa usamaria wowote kwa maana asinge muibia simu asinge kua na haja ya kumfikishia huo ujumbe in the first place. Ni sawa sawa na mtu akuibie pesa halafu aku nunulie chakula na pesa aliyo kuibia. Hauwezi kusema kakufanyia msaada.
   
 6. M

  Msindima JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Anabaki kwenye kundi la wezi hatuna kundi lingine la kumweka,na pia kwa ushauri mwambie rafiki yako akablock line isiendelee tena kutumika.
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Msindima,
  Ameshaiblock hiyo line tayari.
  Na wakati inaibiwa ilikuwa na tshs 5000, nadhani ndo maana jamaa akaendelea kuitumia chip!
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mhhhh!!!!!
  Kwa hiyo mzee kuna wizi wa akili na wenye ubinaadam sio?
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Wezi wa simu mara nyingi hufanya vitendo kama hivi vinavyoonekana vya kiubinadamu kwa vile humo kwenye simu hata hivyo kuna credit! Mara nyingi watu pia wamejua kuhusu ajali au vifo vya watu wao kutokana na ajali baada ya kupigiwa simu na wezi wa hizo simu.All in all tukumbuke kuwa wezi wa simu wengine ni watu kama wewe na mimi hawana alama kuonyesha ni wezi au watu wabaya.
  Hawana utu wala nini.Wangekuwa nao basi wasingeibia wenzao simu.
   
 10. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  huyu ni mwizi lakini kama vile kulivyo na wivu mbaya na wivu mzuri[wa maendeleo]basi na huyu mwizi ni wa kimaendeleo,
   
 11. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2009
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  huyo mwizi alitamani hiyo simu ya jamaa yako hana kingine
  mwombeni arudishe line
   
 12. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Acha kushangaashangaa mwambie awajulishe watu wote waliokuwa na hiyo namba yake, next time huyo msomi mtasikilia kwingine mfano;
  kuna dada aliibiwa pochi yenye simu, card za benki etc asubuhi anaenda kazini, bank card ilikuwa shared na mumewe, kwenye simu namba kaweka majina kama hubby. mama, dada. alichofanya mwizi ni kumtext hubby ampatie password ya bank kwani "ghafla nimeisahau",
  Mke baada ya kuduwaa anampigia hubby nimeibiwa pochi na simu, card, alijibiwa mbona umetext sio muda na nimekupa namba ya siri, hubby kwenda bank imetolewa hela yote!
  Hii unemployment kuna wasomi wengi tu wako mtaani wakishirikiana na wezi. Take care.
   
 13. M

  Msindima JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni kweli usemacho WOS maana nakumbuka hata sisi tulipata taarifa ya kifo cha boss wetu kupitia simu yake,lakini tukirudi kwenye ukweli wala hawana utu kabisa.
   
 14. m

  magneto Member

  #14
  Jul 31, 2009
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  according to principle of excluded middle mwizi mwizi tu hakuna cha nini wala nini
   
 15. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mwizi ni mwizi tu na atapata stahili yake kwa mwenendo huo.
   
  Last edited: Jul 31, 2009
 16. M

  Makanyagio Senior Member

  #16
  Jul 31, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35  Mkuu unanitia shaka, ningekubali hilo kama mwizi huyo angemaliza kuitumia halafu akamrudishia jamaa simu yake. Kutuma SMS ya mtihani sio ishu , hata wale wezi walioiba pesa NBC Moshi waliwafungia watu strong room lakini baada ya kutimua waliwapigia polisi kuwajulisha kuna watu wamefungiwa ndani ili waweze kuokolewa. Kimsingi hapa wao kawakuwa na nia ya kuua ila walitaka pesa tu. Huo utaita ni wizi wa nini?
   
 17. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Wizi ni wizi tu. Ila kama mwizi anaamua kuwa binadamu basi wizi huu tunauita ni wizi wa kulazimishwa siyo wa tabia.

  Ni wizi wa kulazimishwa kwani kama angekuwa na shughuli ya maana ya kumpatia kipato halali cha kununua simu basi asingeiba hii simu. Huyu inaonekana alikuwa na shida ya simu tu, na wala si kibaka. Kibaka akiiba simu cha kwanza ni kuiuza apate hela ya kete.

  Hata hivyo mwizi huyu kwa hatua aliyochukua amehatarisha simu yake aliyoiba, kwani kama jamaa ana namba za kuifunga angeweza kufanya hivyo kwa huduma maalum na simu isingefanya kazi tena.
   
 18. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #18
  Aug 1, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  kuna uwezekano pia huyo sio mwizi ila aliiokota simu jamaa ambayo aliipoteza kwa uzembe wake ndio maana jamaa hakuona sababu ya kumrudishia. Kwahiyo tusimuhukumu kuwa ni mwizi ila huyo jamaa wa mtoa mada ndie alipoteza simu lakini home anasema kaibiwa ili kuficha uzembe wake.
  Ila kama ni mwizi anabaki kuwa mwizi tu ana kundi jingine
   
 19. H

  Heri JF-Expert Member

  #19
  Aug 1, 2009
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 242
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Huu wizi unatia mashaka. Mimi nadhani mwizi anamfahamu mwenye simu na alichukua simu kwa sababu nyigine.
  Hakai akilini mtu kuiba simu na kubaki na sim card na zaidi ya hapo kucheki sms .
  Kuna kitu alikuwa anatafuta.
  Kama mwizi aliwahi kutumia hiyo sim card kupiga simu, chekeni alipiga kwa nani nalabda mnaweza kumpata.
   
Loading...