Huyu ni mume au mzigo?

Mtambuzi haya mambo ya ndoa ni magumu saana.... Unapokua binti mdogo unapata mume kakulea na kukupa lolote utakalo... yaani ni mume in name na vitendo... kahakikisha umeongeza kisomo... kahakikisha kua umepata kazi nzuri yaani yeye anakupa support ya kila namna ambayo yeye kama mume anasatahili na hata beyond that... Ndio maana katika zile marital maneno kuna "For better For Worse".... Maisha yanabadilika... mumeo anaweza fukuzwa kazi au biashara ikaenda vibaya.... Huyo mume hata achukue miaka miwili ama zaidi kuweka mamboa yake sawa na akakutegemea kwa kila kitu.... ana haki na wala sio mzigo.... Na hata kama sio yeye kakuendeleza but in short he is a good man.... then he deserves support from the wife....

N:B Nashukuru kwa kutupa a Break wamama na kuamia kwa Wanaume leo....

Lakini AshaDii, nimesema hivi, anafanya kazi na anapata mshahara, ila mshahara wake anautumia kwa pombe na umalaya au vyoye viwili.... ina maana hata kama amekusomesha na kukutengenezea future jambo ambalo kimsingi ni wajibu wake.......kwa hiyo itakuwa ni halali kwake kutowajibika katika familia na kuelekeza fedha zake katika pombe na umalaya?
 
Kuna msemo huu: "Kazi mbaya kama unayo". Mi nasema, mume mbaya kama unae! Ukiwa na mume, utaimba kila siku kwa mashosti-mara ooh, hajui kazi, mara ooh anahema sana, mara ooh amekuwa bonge siku hizi mara ooh wangu ni mwanaume suruali! Ukiwa unatafuta mume, unaenda hata kwa waganga wakienyeji wakuongezee masaburi ili upendeze na watu wakuoe!! Ndio maisha, hatujui thamani ya kitu mpaka kipotee/kiondoke!
 
Kweli shetani wa mtu ni mtu mwenyewe sikatai kuna familia nyingi zinazoishi katika maisha kama haya ila ukweli sifurahishwi na hizi tabia naomba Mungu atuepushe na hii tabia
 
Back
Top Bottom