Huyu ni msanii wa kiume..

Huyu ni msanii wa kiume..

Jobless_Billionaire

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2022
Posts
3,903
Reaction score
9,915
Hakika zama zimebadilika sana.

Katika kupita mtandaoni nikakutana na picha ya msanii Platform.. Imenifikirisha sana. Itafikia muda sasa jinsia ya kiume kuwa na mionekano ionekane ni sahihi tu kutokana na wasanii wetu kujianika na mionekano kama hii.

Najua sio huyu tu, hata wewe huenda umewahi kukutana na picha za wasanii wengi tu wakiwa na mionekano ya kike. So sad..
1000098554.jpg

Tuliwahi kuishi tukiamini wasanii ni vioo vya jamii kutokana na nguvu waliokuwa nayo katika kuonya, kukosoa na hata kuhimiza maadili yaliyo mazuri.
Hatukatai mziki ni biashara lakini kwa mwenendo uliopo sasa, wasanii ndio wanakuwa kichocheo cha kuibomoa kabisa jamii sababu haohao huimba vitu vya kuchochea ngono, matumizi ya dawa za kulevya, matusi, pombe na mengine mengi kubwa zaidi ni Ushoga na Usagaji.

Wasanii wa sasa huenda mbali zaidi kwa kuihadaa jamii kwa mtindo feki wa maisha wanaouishi. Inawezekana ikaonekana ni kawaida kwa mtu ambaye amepevuka kiakili kung'amua mambo na kutambua huu sio uhalisia, ila wapo ambao bado akili zao hazijawa na nguvu ya kupembua mambo au mengi hawajayatambua kuhusu wasanii ndio huwa rahisi kuhadaika. Mfano wanafunzi (jinsia zote) huweza hata kuamua kusitisha masomo wakiamini muziki unalipa sana kwa kuwa kaona msanii fulani anaishi maisha ya juu sana mtandaoni au anaonekana kumiliki pesa ndefu kwa maisha yake ilhali kiuhalisia kabisa kuna watu wana majina ila uchumi mbovu kabisa. Simaanishi hakuna wenye maisha halisia, wapo lakini asilimia kubwa wanapretend.

Kuna baadhi ya wasanii katika mahojiano yao wamewahi kukiri wazi kuwa hawatamani watoto wao waje kuwa wanamuziki. Hii inadhihirisha wazi kuwa, kama mzazi hafurahii mwanae kuyaishi mambo yaliyopo kwenye game ambayo yeye yumo. Wadada hufanyiwa vitendo vibaya kwa ahadi za kusaidiwa, wavulana pia hutendwa vivyo hivyo kwa ahadi za kutolewa.

Ni hayo tu.
 
Mziki wa Bongo kwasasa unaharibu taswira na mustakabali wa jamii na utamaduni uliopo....

Serikali waendelee kucheka cheka badala ya kuanza kukemea na kutoa adhabu Kali kwa wanaporomosha maadili kwa makusudi....

Au bado wapo kwenye nyumba za ibada na majukwaa wanatupiana maneno kama watoto?
 
Mziki wa Bongo kwasasa unaharibu taswira na mustakabali wa jamii na utamaduni uliopo....

Serikali waendelee kucheka cheka badala ya kuanza kukemea na kutoa adhabu Kali kwa wanaporomosha maadili kwa makusudi....

Au bado wapo kwenye nyumba za ibada na majukwaa wanatupiana maneno kama wajinga au watoto?
Mkuu inashangaza sana. Baraza la sanaa lipo lakini kazi kudeal na wanaoikosoa serikali tu
 
Mziki wa Bongo kwasasa unaharibu taswira na mustakabali wa jamii na utamaduni uliopo....

Serikali waendelee kucheka cheka badala ya kuanza kukemea na kutoa adhabu Kali kwa wanaporomosha maadili kwa makusudi....

Au bado wapo kwenye nyumba za ibada na majukwaa wanatupiana maneno kama wajinga au watoto?
Maadili yenu wabongo yameandikwa wapi??
Ni wapi huyo platform anaweza kushtakiwa kwa kuvunja maadili, kakosea kip??

Mnaweza kua mnapigania kitu ambacho hakipo.
 
Avatar uliyo nayo inasadiki kilichopo kwako...

Maudhui yanayotolewa na kuonyeshwa na mnaowaita wasanii yanaridhisha
Leo nimekaa na mwanangu wa kike anaimba nyimbo za hovyo, kavaa hovyo anakuambia ni fashion
 
Sawa. Mpelekee mwanao wa kiume zawadi ya gauni na wewe jinunulie abaya na hereni Poor Brain
Lete hoja sio viroja, tamaduni zenu zimeandikwa wapi??

Zinaharibiwa, zinaharibiwaje? Inasema hivi huyu kaharibu hivi nk.

Na kuhusu magauni si wanavaa wanaume wengi tu, je wanashitakiwa? Wanapigwa? Wanakemewa?
Ni wanaume wangapi wanavaa hereni? Wameshitakiwa, wamepigwa. Serikali haioni hayo? Basata haioni hayo? Vipi inakemea, inashauri au walau inaonya???

Ndio maana nikawaambia isijekua mnapambania kitu ambacho hamna.
 
Hakuna zilipoandikwa. Ila fanya nilichokueleza
 
Avatar uliyo nayo inasadiki kilichopo kwako...

Maudhui yanayotolewa na kuonyeshwa na mnaowaita wasanii yanaridhisha
Leo nimekaa na mwanangu wa kike anaimba nyimbo za hovyo, kavaa hovyo anakuambia ni fashion
Ujue shida yenu mnatumia hisia na sio akili.
Huyo mwanao wa kike kuimba hizo nyimbo ni kosa la msanii au lako mzazi??

Na unajiita baba kabisa??
 
Hakuna zilipoandikwa. Ila fanya nilichokueleza
Kama hakuna zilipoandikwa unasemaje anazikiuka??
Mlikubaliana wapi kua hizo ndio tamaduni zenu?

Hebu nipe tamaduni ya kwanza mpaka ya mwisho??

Tumia akili sio hisia dogo, kuna mmoja hapo toto lake linaimba nyimbo za Zuchu halafu anamlaumu Zuchu na sio kua ni kosa lake yeye kuruhusu hizo nyimbo kupigwa hovyo nyumbani kwake, kuruhusu mwanae aende mahali ambako hizo nyimbo zinapigwa .

Umemfollow platform au page za hovyo, unakuja kulalamika maadili ilhali wewe ndie unaetafuta kuyavunja hayo maaddili.
 
Wewe kavae madera, vitenge na vikuku. I'm done
 
Hakika zama zimebadilika sana.

Katika kupita mtandaoni nikakutana na picha ya msanii Platform.. Imenifikirisha sana. Itafikia muda sasa jinsia ya kiume kuwa na mionekano ionekane ni sahihi tu kutokana na wasanii wetu kujianika na mionekano kama hii.

Najua sio huyu tu, hata wewe huenda umewahi kukutana na picha za wasanii wengi tu wakiwa na mionekano ya kike. So sad..
View attachment 3360347

Tuliwahi kuishi tukiamini wasanii ni vioo vya jamii kutokana na nguvu waliokuwa nayo katika kuonya, kukosoa na hata kuhimiza maadili yaliyo mazuri.
Hatukatai mziki ni biashara lakini kwa mwenendo uliopo sasa, wasanii ndio wanakuwa kichocheo cha kuibomoa kabisa jamii sababu haohao huimba vitu vya kuchochea ngono, matumizi ya dawa za kulevya, matusi, pombe na mengine mengi kubwa zaidi ni Ushoga na Usagaji.

Wasanii wa sasa huenda mbali zaidi kwa kuihadaa jamii kwa mtindo feki wa maisha wanaouishi. Inawezekana ikaonekana ni kawaida kwa mtu ambaye amepevuka kiakili kung'amua mambo na kutambua huu sio uhalisia, ila wapo ambao bado akili zao hazijawa na nguvu ya kupembua mambo au mengi hawajayatambua kuhusu wasanii ndio huwa rahisi kuhadaika. Mfano wanafunzi (jinsia zote) huweza hata kuamua kusitisha masomo wakiamini muziki unalipa sana kwa kuwa kaona msanii fulani anaishi maisha ya juu sana mtandaoni au anaonekana kumiliki pesa ndefu kwa maisha yake ilhali kiuhalisia kabisa kuna watu wana majina ila uchumi mbovu kabisa. Simaanishi hakuna wenye maisha halisia, wapo lakini asilimia kubwa wanapretend.

Kuna baadhi ya wasanii katika mahojiano yao wamewahi kukiri wazi kuwa hawatamani watoto wao waje kuwa wanamuziki. Hii inadhihirisha wazi kuwa, kama mzazi hafurahii mwanae kuyaishi mambo yaliyopo kwenye game ambayo yeye yumo. Wadada hufanyiwa vitendo vibaya kwa ahadi za kusaidiwa, wavulana pia hutendwa vivyo hivyo kwa ahadi za kutolewa.

Ni hayo tu.
Utakuta anatoa na huduma nyingine huyu jamaa
 
Back
Top Bottom