Tumwesige senior
JF-Expert Member
- Jan 28, 2013
- 5,863
- 10,344
Itakuwa alishavuliwa ubingwa huyo
Gen z wa Tanzania haoHakika zama zimebadilika sana.
Katika kupita mtandaoni nikakutana na picha ya msanii Platform.. Imenifikirisha sana. Itafikia muda sasa jinsia ya kiume kuwa na mionekano ionekane ni sahihi tu kutokana na wasanii wetu kujianika na mionekano kama hii.
Najua sio huyu tu, hata wewe huenda umewahi kukutana na picha za wasanii wengi tu wakiwa na mionekano ya kike. So sad..
View attachment 3360347
Tuliwahi kuishi tukiamini wasanii ni vioo vya jamii kutokana na nguvu waliokuwa nayo katika kuonya, kukosoa na hata kuhimiza maadili yaliyo mazuri.
Hatukatai mziki ni biashara lakini kwa mwenendo uliopo sasa, wasanii ndio wanakuwa kichocheo cha kuibomoa kabisa jamii sababu haohao huimba vitu vya kuchochea ngono, matumizi ya dawa za kulevya, matusi, pombe na mengine mengi kubwa zaidi ni Ushoga na Usagaji.
Wasanii wa sasa huenda mbali zaidi kwa kuihadaa jamii kwa mtindo feki wa maisha wanaouishi. Inawezekana ikaonekana ni kawaida kwa mtu ambaye amepevuka kiakili kung'amua mambo na kutambua huu sio uhalisia, ila wapo ambao bado akili zao hazijawa na nguvu ya kupembua mambo au mengi hawajayatambua kuhusu wasanii ndio huwa rahisi kuhadaika. Mfano wanafunzi (jinsia zote) huweza hata kuamua kusitisha masomo wakiamini muziki unalipa sana kwa kuwa kaona msanii fulani anaishi maisha ya juu sana mtandaoni au anaonekana kumiliki pesa ndefu kwa maisha yake ilhali kiuhalisia kabisa kuna watu wana majina ila uchumi mbovu kabisa. Simaanishi hakuna wenye maisha halisia, wapo lakini asilimia kubwa wanapretend.
Kuna baadhi ya wasanii katika mahojiano yao wamewahi kukiri wazi kuwa hawatamani watoto wao waje kuwa wanamuziki. Hii inadhihirisha wazi kuwa, kama mzazi hafurahii mwanae kuyaishi mambo yaliyopo kwenye game ambayo yeye yumo. Wadada hufanyiwa vitendo vibaya kwa ahadi za kusaidiwa, wavulana pia hutendwa vivyo hivyo kwa ahadi za kutolewa.
Ni hayo tu.