Huyu ndugu yangu wa damu ananitia aibu sana kwa ulevi uliokithiri

Hamjambo???

Niende kwenye mada;-

Nina ndugu yangu wa kiume(27) , yani ni mlevii haifai, akishaanza kunywa atahakikisha anakunywa hadi pesa aliyokuwa nayo inaisha yote.

Sasa aibu inakujaje;? Akishalewa kwanza anakuwa na maneno flan yasiyofaa,ya hovyo hovyo, ya aibu aibu yakutia aibu sana

Akilewa tu yan ni lazima aje eneo langu La biashara kupiga vizinga ama kuzuga hapo kisha anaondoka, ataongea ongea hapo maneno ya ovyo ovyo, Mara alale chini, Mara aandike andike chini, yan ni shida.

Kama kuna mtu yeyote anayefahamu dawa ya kuacha pombe aje atusaidie wapendwa wetu nao waache coz wanashindwa hata kufanya maendeleo,kipato choote kinaishia kwenye pombe.
dawa ipo ila unaelekezwa unamtengenezea ww mwenyewe na inachanganywa n pombe
 
Mpaka siku akatwe malinda ndio ataona madhara ya kulewa kijinga jinga.

Mwambie ukweli akiwa mzima kwamba hutaki mtu mlevi,akirudia kulewa fungua ktk banda la mbwa alale humo akiamka asubuhi unamtaarifu kwamba kila akilewa atalala humo.
 
nlikuwa na ndugu alikuwa mlevi chakari , siku moja nlipomchoka nlipanga njama na rafiki ninayemwamini kufa , tulimtegea njiani , tulichukua mix ya mayai viza na santo , alikuwa na tabia ya kulala njiani , usiku alipopitwa tulimpaka kwenye matacore na suruali , bro alipogutuka kesho alijua mpaka leo kwamba aliliwa tigo kulingana na harufu , yeye na pombe hadi leo ni maadui wakubwa
Nauza mikate! Nauza mikate!
 
Hilo ni pepo muombee sana maana halitamuua lakini litamkosesha mengi
Unasema kweli Mshana hata mimi nina ndugu yangu yuko kwenye late 40s yani pombe imemtoa kwenye reli hadi kazi kafukuzwa afya yake mbaya. Sasa hivi anaishi na mama yake anamlea kama mtoto tu maana yeye ni kula kulala watoto asomeshewe hana hata wazo lolote akiumwa atibiwe akipata pesa kidogo pombe tu.
 
Usije kuta kuna kitu cha kuvuta biashara umetumia kinamfanya hivyo.. kwanini aje dukani kugalagala?
 
Hamjambo???

Niende kwenye mada;-

Nina ndugu yangu wa kiume(27) , yani ni mlevii haifai, akishaanza kunywa atahakikisha anakunywa hadi pesa aliyokuwa nayo inaisha yote.

Sasa aibu inakujaje;? Akishalewa kwanza anakuwa na maneno flan yasiyofaa,ya hovyo hovyo, ya aibu aibu yakutia aibu sana

Akilewa tu yan ni lazima aje eneo langu La biashara kupiga vizinga ama kuzuga hapo kisha anaondoka, ataongea ongea hapo maneno ya ovyo ovyo, Mara alale chini, Mara aandike andike chini, yan ni shida.

Kama kuna mtu yeyote anayefahamu dawa ya kuacha pombe aje atusaidie wapendwa wetu nao waache coz wanashindwa hata kufanya maendeleo,kipato choote kinaishia kwenye pombe.
MkUU, Huyu sio ndugu yako unamuombea Ushauri dawa ya kuacha pombe, huyu ni wewe unazunguka zunguka kijanja upate ushauri wa namna ya kuacha pombe!

PoLE SaNA, pombe ni mbaya, ila ni tamu, binafsi naenda wiki pili sasa sijanywa pombe, nikifanikiwa hii weekend ya wiki hii kutoboa bila kunywa pombe basi alhamdullillah nitakuwa nimefanikiwa kuacha kabisa maana ilikuwa haipiti siku moja bila kulewa bia za elfu 30 mpaka 60!

Nimeweka nia na dhamira ya dhati kuikataa pombe, najiepusha sana vishwawishi ikiwapo marafiki wa gambe, nasoma sana kitabu takatifu sahivi, nasoma pia vitabu vingine, nacheza games na kujikip bize na mambo mengine mengine ili nisipate muda wa kuwa idle nikajikuta natafuta bar ilipo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom