Huyu ndiye Waitara aliyeikimbia CHADEMA

Huyu ndiye Waitara aliyeikimbia CHADEMA

Kama ulimfuatilia vizuri wakati anahama alisema mwenyewe kuwa anatamani kuwa waziri kamili uone akili na matamianio yake yako wapi

Umeandika nini hiki! Kwani upinzani hautamani kushika dola? Wewe binafsi hutamani yaliyo mazuri!
 
Sawa mkuu, hao hawana hadhi tena ya kuongoza taifa. Ni bora hawa ambao makabila yote yamo chamani japo sio kwamba hawana madhaifu sio hawa ambao ni jamii moja na ubinafsi wao ndio tuwape nchi. Nasema haitatokea.
Mbona yote yapo pia kwao,sugu,Pro j,msigwa,heche,nk
 
Sawa mkuu, hao hawana hadhi tena ya kuongoza taifa. Ni bora hawa ambao makabila yote yamo chamani japo sio kwamba hawana madhaifu sio hawa ambao ni jamii moja na ubinafsi wao ndio tuwape nchi. Nasema haitatokea.
Kukiwa na katiba mpya,tume huru, nk ni haki nao kupewa walishindwa hupewa wengine ndo Democraticy iliyo hakuna mwenye hatimiliki.
 
Hapana kaka, watu mbali na jamii yao ni wachache sana sana sana.
 
Kukiwa na katiba mpya,tume huru, nk ni haki nao kupewa walishindwa hupewa wengine ndo Democraticy iliyo hakuna mwenye hatimiliki.
Sawa mkuu huu ndio Uhuru wa kuongea, hatuwezi kufanana kimawazo.
 
Sawa mkuu huu ndio Uhuru wa kuongea, hatuwezi kufanana kimawazo.
Sawa, wangekuwa hawafai wasingerudishwa kundini na kupewa teuzi,na kuachwa wale asili wafia chama.Mtulia,Mollel,Kafulila, Machari,nk kwa uchache.tafsiri yake wanafaa wakipata nafasi
 
Ni kweli kabisa lakini point yangu ni kwamba, upande wa pili bado kabisa hawaja qualify kupewa taifa waliongoze kwa sababu ya hulka na sifa za viongozi wao wakuu wa chama. Ni watu walio kumbatia umimi( u_sisi) ila nakubali kwamba wanao viongozi makini wachache wasio na ubinafsi wa maslahi binafsi.
 
Sawa mkuu, hao hawana hadhi tena ya kuongoza taifa. Ni bora hawa ambao makabila yote yamo chamani japo sio kwamba hawana madhaifu sio hawa ambao ni jamii moja na ubinafsi wao ndio tuwape nchi. Nasema haitatokea.
daaa kwa point hiii uliyoandika watakuchukia mkuu
 
Atagombea tena ukonga, cha msingi tu hatutaki kusikia tena wanatupigia kina akwilini wasio na hatia wamalizane wenyewe.Maadamu washaamua kuchezea kodi zetu zisizo na kazi ya kufanya Zaid ya kuchezewa na wanasiasa.
 
Mbona hujasema marehemu ameacha nini?. Au hakua na chochote.
 
MWITA MWIKWABE WAITARA amezaliwa Kijiji cha Kangaliani, Tarafa ya Ingwe, Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Julai 17, 1976.

Alisoma shule ya msingi kijijini kwao hadi darasa la nne, akahamia Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mahojiano yake mbalimbali na vyombo vya habari na pia wasifu wake katika tovuti ya Bunge, shuleni hakuwa ameandikishwa na wazazi wake, alikwenda mwenyewe.

Baba yake alikuwa mfugaji, mkulima na mwindaji pia, mtazamo wake ulikuwa aangalie mifugo na si masuala ya shule.
Alipofika umri wa kuanza shule alizuiliwa ili achunge ng’ombe na kwa sababu kaka zake hawakuwapo, ikabidi lazima aangalie mifugo. Kutokana na baba yake kutompeleka shule, hakuwa na sare hali iliyofanya achapwe sana. Mwalimu Mkuu alikuwa rafiki wa baba yake.

Hali hiyo ilimfanya ahamie kwa babu yake na huko baba yake mdogo alimnunulia sare, akaendelea na shule.
Aliacha shule akiwa darasa la nne, akaenda Nyamongo kwenye machimbo ya dhahabu, akapata fedha akajenga nyumba ya msonge na mwaka 1993 akahamia Dar es Salaam, akaishi Kipunguni kwa kaka yake akifuga kuku, alikaa hapo Machi hadi Agosti mwaka 1993.

Alihamia kwa baba yake mdogo Mtoni Mtongani baada ya kuona kaka yake hana nia ya kumsomesha na huko akapata nafasi ya kuendelea na shule katika Shule ya Msingi Mtoni Kijichi, akaendelea na darasa la sita baada ya kupata uhamisho kutoka kijijini kama mwanafunzi mtoro.

Alisoma akipata msaada wa walimu wake kwenye masuala ya fedha na mahitaji mengine ya shule. Alifaulu la saba na kuingia Shule ya Sekondari Azania, aliposoma hadi kidato cha sita kuanzia mwaka 1995 hadi 2001.

Wakati huo akijitegemea kwa kuuza karanga, mayai ya kuchemsha na kusomesha masomo ya ziada.

Baada ya kumaliza kidato cha sita alilazimishwa kurudi nyumbani kuoa, alikwenda kuoa baada ya mvutano mkali na kukaa mwezi mmoja na mke kisha majibu yalitoka amefaulu kuingia Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) alikosoma mwaka 2002 hadi 2006 na kupata Shahada ya Kwanza (BA).

Alimuacha mkewe baada ya kukataa kurudi kijijini ili yeye aendelee na masomo. Aliondoka akiwa mjamzito, akajifungua akiwa huko ambaye sasa yupo sekondari. Maisha ya Siasa Waitara aliingia katika siasa kwa mara ya kwanza akiwa anasoma Shule ya Sekondari Azania mwaka 1998.

Alijiunga CCM baada ya kushawishiwa kwenye mkutano wa Sofia Simba na Iddi Simba waliofika shuleni kwao.
Waitara aliyewahi kuongoza mgomo wa wanafunzi mwaka 2002 akiwa UDSM na kusababisha chuo kufungwa, aliwahi kuwa Katibu wa UVCCM Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam na baadaye kuhamishiwa Tanga kwa nafasi hiyo hiyo na kupanda ngazi kuwa Katibu wa UVCCM Mkoa wa Tanga.

Alihamishiwa Dar es Salaama awe Msaidizi wa Mwenyekiti UVCCM Taifa, lakini aliona ni udhalilishaji kutokana na kutokuwa na nafasi tena ya kuingia vikao vya maamuzi, akahama chama hicho na kuingia Chadema.

Kutokana na mwaka huo 2008 kushiriki vizuri kampeni za ubunge Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Tarime baada ya mbunge wake, Chacha Wangwe kufariki dunia, aliteuliwa kuwa Ofisa wa Sera na Utafiti wa Chadema hadi 2014.

Lakini mwaka 2010 aligombea ubunge wa Tarime kwa tiketi ya Chadema na kwa bahati mbaya kutokana na ushindani wa mbunge wa awali kupitia Chadema kuhamia CUF, kura hazikutosha na alishinda mgombea wa CCM, Nyambari Nyangwine kwa tofauti ya kura 730.

Waitara aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivule mwaka 2014 (wakati huo katika Kata ya Kitunda – sasa Kata ya Kivule), aligombea ubunge mwaka 2015 Jimbo la Ukonga akashinda kwa zaidi ya kura 90,000 dhidi ya mgombea wa CCM, Jerry Silaa, nafasi aliyoitumikia hadi jana aliporejea CCM; na sasa uchaguzi utalazimika kufanyika tena Ukonga kujaza nafasi hiyo aliyoiacha.
Sawa mkuu
 
usiwe na hasira sana hiyo ndio demokrasia
IMG_20180730_123843.jpg
 
Back
Top Bottom