Huyu ndiye simba wa CHADEMA

Huyu ndiye simba wa CHADEMA

kisugujira

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2012
Posts
774
Reaction score
200
"Nchi yetu kwa muda mrefu imekuwa ni kisima cha amani na mfano wa kuigwa. Lakini sasa hivi kuna ufa umetokea nchini hakuna amani. Wakristo na waislamu wameishi kwa kuheshimiana na kwa upendo kwa muda mrefu. Hivi karibuni kumekuwepo na chokochoko za kidini. Makanisa yanachomwa moto, mapadri, wachungaji na waumini wanauawa.

Chama Cha Wananchi CUF kiliitwa ni chama cha kiislamu! Sasa hivi CHADEMA kinasemwa ni chama cha kikristo! Haya yote yanasemwa na serikali na wabunge wa CCM bungeni yakilenga kujenga hofu na kuleta chuki kwa wabunge wa upinzani na wananchi.''

Maneno hayo yalisemwa na Mh.Zito Kabwe wakati wa mjadala wa wizara ya mambo ya ndani baada ya tukio la kusikitisha na kutisha lililotokea Arusha. Aliomba liundwe azimio litakalokemea na kupinga kauli za chuki (hate speeches) toka kwa wabunge wa CCM kwenda kwa wabunge wa vyama vya upinzani bungeni.

Pia alipendekeza mihadhara ya kidini yenye kuleta na kuchochea chuki ipigwe marufuku nchini, huku akisisitiza upendo na umoja kwa kusema, "Sisi sote ni ndugu. Linapokuja swala linalohusu maslahi ya Taifa,tofauti za vyama, dini na ukabila yatupasa kuvitupilia mbali."

Leo hii azimio hilo na mambo mengine yenye manufaa kwa Taifa yamepigiwa kura na kuungwa mkono na wabunge wote bungeni Dodoma, huku Mh. Dr Augustino Lyatonga Mrema, akitoa siku saba za kukomesha mihadhara yote ya kidini hapa nchini.
 
Kweli haina haja tena ya mihadhara, watu wakafundishwe ktk nyumba zao za ibada
 
Na viredio vya kidini na vya binafsi viwe-monitored maana vingine vinakera mno.
 
Kisugujira,

Nimejaribu ku -relate Heading na What is in nimeshindwa totally, sijui umemaanisha nini
 
kweli kabisa mihadhara yote ya kidini ipigwa marufuku kabisa kwa sababu haina tija kwa taifa letu.
 
Kweli haina haja tena ya mihadhara, watu wakafundishwe ktk nyumba zao za ibada

hivi kuna tofauti yoyote kati ya mihadhara na mikutano ya injili?? lugha inanisumbua
 
Je na radio na tv za dini/madhehebu nazo zifungwe?maana naona bado mijadala itahamia kwenye tv/radio na bado italeta chokochoko
 
"Nchi yetu kwa muda mrefu imekuwa ni kisima cha amani na mfano wa kuigwa. Lakini sasa hivi kuna ufa umetokea nchini hakuna amani. Wakristo na waislamu wameishi kwa kuheshimiana na kwa upendo kwa muda mrefu. Hivi karibuni kumekuwepo na chokochoko za kidini. Makanisa yanachomwa moto, mapadri, wachungaji na waumini wanauawa. Chama Cha Wananchi CUF kiliitwa ni chama cha kiislamu! Sasa hivi CHADEMA kinasemwa ni chama cha kikristo! Haya yote yanasemwa na serikali na wabunge wa CCM bungeni yakilenga kujenga hofu na kuleta chuki kwa wabunge wa upinzani na wananchi.'' Maneno hayo yalisemwa na Mh.Zito Kabwe wakati wa mjadala wa wizara ya mambo ya ndani baada ya tukio la kusikitisha na kutisha lililotokea Arusha. Aliomba liundwe azimio litakalokemea na kupinga kauli za chuki (hate speeches) toka kwa wabunge wa CCM kwenda kwa wabunge wa vyama vya upinzani bungeni. Pia alipendekeza mihadhara ya kidini yenye kuleta na kuchochea chuki ipigwe marufuku nchini, huku akisisitiza upendo na umoja kwa kusema, "Sisi sote ni ndugu. Linapokuja swala linalohusu maslahi ya Taifa,tofauti za vyama, dini na ukabila yatupasa kuvitupilia mbali."Leo hii azimio hilo na mambo mengine yenye manufaa kwa Taifa yamepigiwa kura na kuungwa mkono na wabunge wote bungeni Dodoma, huku Mh. Dr Augustino Lyatonga Mrema, akitoa siku saba za kukomesha mihadhara yote ya kidini hapa nchini.
daah, maamuzi magumu hadi lipigwe guruneti kumlenga balozi?Mlikuwa hamjui vurugu ikikomaa; hakuna posho! Hakuna vikao wala washa...?
 
Mtoa mada acha unafiki, mbona vipande hivi hapa umeviacha, ZZK kaugusa "mfumo" tunaolalamikia waislamu....

Mheshimiwa Mwenyekiti, waislam na wakristo nchi hii hawana chuki kwa sababu wanaishi pamoja, ni marafiki, ni ndugu na kama ingekuwa kwa mfano waislam wanawachukia wakristo waislam wangevunja makanisa au wangechoma makanisa au wangewalipua wakristo. Wakati wa tukio la Mwembechai ndipo ambapo Polisi waliingia mskitini wakaua watu, wanawake wakateswa kwenye magereza na kadhalika, watu wakakaa miezi mitano gerezani bila kushtakiwa lakini hapakuwa na mtukio yoyote ya namna hii. Waislam na wakristo wa nchi hii ni wamoja. Wananchi wetu ni wa moja lakini sisi viongozi kwa kutoa kauli ambazo ni "very irresponsible" tunawagawa watu wetu na ni lazima tukatae hali hii. Tunafanya nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, state, dola, ihakikishe inajiondoa kwenye shughuli za uendeshaji wa mambo ya kidini. Ijiondoe kabisa. Kwa mfano kuna lawama ya muda mrefu sana ya waislam kuhusu BAKWATA, Waislamu miaka mingi toka mwaka 1969 wakati Serikali imeunda BAKWATA wanalalamika. Leo hii Serikali ikitaka kuzungumza na waislam inafanya nini? Inaenda kuwaita BAKWATA. Hawana legitimacy ya waislam, hamtaweza ku-addres masuala ya waislam lakini ni rahisi sana kuweza kuongea na CCT kwa sababu CCT ni chombo ambacho kina uhuru wake. Kwa hiyo Serikali ijiondoe kwenye uendesheji wa shughuli za kidini. Hapa ndipo tutakapoweza kuhakikisha kwamba tunakuwa na nchi moja nchi ambayo ina amani.
 
Kisugujira,
Nimejaribu ku -relate Heading na What is in nimeshindwa totally, sijui umemaanisha nini

Duuuuh, pole sana! Lakini ngoja nibonge kidhungu kama wewe. Aah well, I think it's better for you to just read again what has been written and try to find out who's the main character in the thread. Once you discover the main character, you will automatically know who is the real Lion of CHADEMA I'm talking about. And in doing so you will not look a spoon fed oriented man. Always try to think inside and outside of the box. Thank you.
 
Mtoa mada acha unafiki, mbona vipande hivi hapa umeviacha, ZZK kaugusa "mfumo" tunaolalamikia waislamu....
Mheshimiwa Mwenyekiti, waislam na wakristo nchi hii hawana chuki kwa sababu wanaishi pamoja, ni marafiki, ni ndugu na kama ingekuwa kwa mfano waislam wanawachukia wakristo waislam wangevunja makanisa au wangechoma makanisa au wangewalipua wakristo. Wakati wa tukio la Mwembechai ndipo ambapo Polisi waliingia mskitini wakaua watu, wanawake wakateswa kwenye magereza na kadhalika, watu wakakaa miezi mitano gerezani bila kushtakiwa lakini hapakuwa na mtukio yoyote ya namna hii. Waislam na wakristo wa nchi hii ni wamoja. Wananchi wetu ni wa moja lakini sisi viongozi kwa kutoa kauli ambazo ni "very irresponsible" tunawagawa watu wetu na ni lazima tukatae hali hii. Tunafanya nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, state, dola, ihakikishe inajiondoa kwenye shughuli za uendeshaji wa mambo ya kidini. Ijiondoe kabisa. Kwa mfano kuna lawama ya muda mrefu sana ya waislam kuhusu BAKWATA, Waislamu miaka mingi toka mwaka 1969 wakati Serikali imeunda BAKWATA wanalalamika. Leo hii Serikali ikitaka kuzungumza na waislam inafanya nini? Inaenda kuwaita BAKWATA. Hawana legitimacy ya waislam, hamtaweza ku-addres masuala ya waislam lakini ni rahisi sana kuweza kuongea na CCT kwa sababu CCT ni chombo ambacho kina uhuru wake. Kwa hiyo Serikali ijiondoe kwenye uendesheji wa shughuli za kidini. Hapa ndipo tutakapoweza kuhakikisha kwamba tunakuwa na nchi moja nchi ambayo ina amani.

Babu Kijana, nashukuru kwa nyongeza ya maneno yako. Kwani hayo uliyoyaongezea ili WanaJF wayasome na kuyachambua ni mwendelezo wa kile nilichokiandika na siyo kukianzisha. Simba wa CHADEMA Mh. Zito Kabwe ndiye aliyekianzisha bungeni kwa manufaa ya Taifa.

Tengua kauli yako manake sijajua kwa nini umeniita mnafiki! Daima kumbuka hate speeches hazitakiwi.
 
Hongera @ Prince Tumbo- watu wanadhani amani ni wimbo kumbe ni matendo yanayozingatia haki na utu wa mtu au kundi la watu. Amani siyo utulivu kama wengi wetu tusiotaka kufikiri tunadhani. Utulivu unaukomo wake hasa aple waliotulizwa kwa nguvu watachoka na kudai haki. Ikiwa kweli tunataka amani kama tunavyoiimba kila siku hasa kwa wale wanaoona uislam ndo chanzo cha dalili za kukosekana huo utulivu unaoitwa amani bbaada ya uvumilivu kuanza kuwatoka, basi wafanye hima kuwashauri hao wanaoona wanahubiri amani wafanye hivyo kutoka mioyoni mwao si tu kwenye ndimi zao. Mara ngapi makanisa yametoa lugha ya kuchukiza lkn hakuna anayeinua mdomo kusema lolote? Ebu tuwe wakweli wa maneno na mioyo yetu ili kunusuru nchi yetu. Tuache unafiki
 
Back
Top Bottom