Tanzania matatizo sugu ambalo ni udini ambalo limetuletea
1.migawanyiko katika jamii
hakuna tena umoja wa kitaifa imebaki "wao na sisi" raisi anachagua viongozi wakuu wa serkali kwa kuangalia imani za dini kuliko uwezo wao wa utendaji kazi, viongozi wabovu wana support kubwa kutoka kwa wananchi wenye imani moja. Misemo kama "sasa ni zamu yetu" inasikika mitaani ikisemwa na wananchi wa kawaida, wengi wao hawana unafuu wowote kiuchumi.
2. Mamlaka makubwa ya raisi
katiba iliyopo inampa mtu mmoja madaraka kupita kiasi hasa uteuzi wa watumishi wa serkali na idara zake. fikira kila mfanyakazi mwenye cheo cha ukurugenzi na kwenda juu ni mteule wa rais, hii inasababisha viongozi kujipendekeza na kushindwa kufanya kazi kulingana na taaluma zao, hawawajibiki kwa wananchi wanaowatumikia bali kwa bwana wao aliowateua "pangu pakavu phenomenon" katiba mbovu namna hii inampa rais nafasi nzuri tu ya kuweka kila kona watu anaowapenda, hii siyo hali nzuri hasa kipindi hiki ambako jamii inaendelea kupasuka kwa misingi ya dini. rais anaweka madarakani watu wa kundi lake na katiba inamruhusu
3. Udhibiti wa uraia
nchi ambayo haijui nani ni raia au siyo raia wake haiwezi kuendelea hata kidogo, maendeleo huja kwa kazi ngumu na unchungu wa wananchi kuziendeleza na kusimamia raslimali zao. wasimamizi wa raslimali zetu wanatajwa kuwa wamalawi, wasomali, wacongo, wanyarwanda, warundi nk nk huku wamiliki wa biashara kubwa kubwa ni wahindi na waarabu. To be honest tanzania ni nchi pekee duniani ambako watu ambao siyo raia wanamiliki uchumi wa nchi na ni viongozi wa ngazi za juu serkalini. Hii hali inachangiwa sana na udini maana, mmatumbi anamwona mpakistani kuwa ndugu yake wa karibu zaidi kuliko mmatumbi wenzie anaetofautiana nae kiimani.
3. Ujinga wa wananchi
Dini zingine zinachangia kwa kiasi fulani kuwakosesha watanzania elimu bora, sehemu kubwa ya jamii ya kitanzania bado ni mbumbumbu. Ujinga wa watanzania ni mtaji mkubwa kwa wageni na watawala dhalimu na ni hatari kwa raslimali za nchi
UDINI UNAIMALIZA TANZANIA