Kuhusu mambo ya Mungu sipendi kuingilia sana lakini Lowassa amechoka sana kwa sasa, wanaoweza kumwona kwa macho yao na kukaa naye kwa muda wataelewa nasema kitu gani, kama Mungu anaweza kumrudishia ujana wake lingekuwa jambo la Neema sana kwake maana najua angependa sana aende Magogoni. Nina imani kikubwa anachoangalia kwa sasa ni hao watakaoshika nchi wachunge masilahi yake aliyowekeza kila kona ya nchi hii, watoto, wajukuu zake waweze kufaidi siku yake itakapofika ambayo siijui... anaweza kujaliwa kuishi hadi miaka zaidi ya 100 na tukaenda kumtembelea hata haoni tena.