Innocenthezron
JF-Expert Member
- Oct 13, 2016
- 393
- 469
VLADMIR V. PUTIN
Achana na huyu mtu asee, ukiachana na ukweli kwamba ni msomi ila pia afisa usalama wa zamani hiki kichwa kina hesabu kubwa sana..
Baada ya Obama na wenzake kumtuhumu kuingilia na kudukua taarifa mbalimbali zinazokihusu chama cha Democratic na kupelekea chama hicho kushindwa uchaguzi, leo Obama kawafukuza wanadiplomasia wa Urusi wapatao 35 na familia zao kama vikwazo dhidi yao kwa kuhusika na udukuaji huo..
Dunia ikiwa inasubiri kwa hamu kuona Urusi watachukua hatua gani na wakati huo wizara ya mambo ya nje ya Urusi ikiwa imependekeza na kumshauri Putin juu ya kulipiza, Putin amesema hatamfukuza mmarekani yeyote nchini Urusi.
Hatua hii imewashangaza sana wengi lakini Putin akiwa anajua kabisa uongozi wa Oboma umebakiza wiki tatu tu uondoke hivyo wanachokifanya ni kujaribu kuficha aibu ya udhaifu wa uongozi wake na kushindwa kwa mgimbea waliemtaka na siku si nyingi ataingia madarakani rais anaeonekana yuko tayari kurejesha uhusiano mzuri kati ya Urusi na Marekani, Putin ameamua kuachana na hatua za kulipiza mpaka pale Trump atakapokua kaingia madarakani na kuona ni jinsi gani rais huyu mpya atakavyolishughulikia hili swala..
Obama hana anachoweza kukifanya cha maana kwa wiki tatu zilizobaki, kinachoendelea ni sawa na mtu uliempiga katika kila ugomvi wenu akaamua kua anachukua mawe anaponda juu ya bati lako kama njia ya kujiliwaza na kuupoza moyo...