Ninachokiona pekee kwa mleta uzi ni kukosa "exposure". Hawa watu weupe ni social kweli kweli na ni LAZIMA usome vizuri utamaduni wao ili uishi nao vizuri. Sio sawa na kina "koku" au "mwajuma ndala ndefu" wa huku kwetu(sorry girls dont feel offended) ambao wamebanwa na miiko ya tamaduni za kiafrika kiasi ambacho hawezi kukufanyia baadhi ya mambo unless muwe wapenzi. Wenzetu weupe hata anaweza kukiss shavuni na bado akawa hamaanishi mapenzi hayo unayofikiria wewe. Lakini pia weupe hawa ni wawazi sana, kama amekupenda atakwambia tu kweupeeee. Hebu focus on your job, tena piga kazi kisawasawa kiasi hata muda wake wa kuondoka aweze kukurecomend kuchukua nafasi yake au pengine uhamishiwe huko alikotoka/atakakokwenda yeye. Kwa hiyo wewe piga kazi na boresha uhusiano wako wa kikazi na yeye. Jikaze, msemee "dula kichwa wazi "atulie.
Kingine jitahidi na wewe kuwa na time yako, sio kila akikwambia njoo basi huyooooo, sometimes jipe thamani, hata kama utakwenda ila usimpe jibu la moja kwa moja angalau aone na wewe ni mtu smart, waweza mwambia utaangalia schedule yako ilivyo then utamjulisha kama uko na muda. Sio akikwambia lets meet at home saa fulani, wewe ni YES YES YESSSS nyiiiingi. Value yourself dude! Hii ndio nafasi ya kukua kikazi, ipiganie learn alot from her.
Kingine hebu usiache mbachao kwa msala upitie, huyo binti anaekufatafata wa kiswahili, hebu mchukulie serious na usivutike na material things za mzungu! Ikiwezekana oa huyo mswahili na focus kwenye kazi. Utakuwa umeepukana na vishawishi.