Huyu mzee tuliempangisha amebadilika sana kauli zake wakati hajapata nyumba

chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
6,515
15,691
Wanabodi,

Huyu mzee tumempangisha nyumba yetu ya jijini Dar, kama familia tulimuona ni mwenye busara sana alikua na kauli nzuri, alikua ananyenyekea sana kwa watu, alijitambulisha kama mnyonge lakini amebadilika, majirani anawatukana hovyo kisa yeye anakula nyama, anaona yeye kupangishwa nyumba nyeupe ya ufukweni ni bora zaidi. Anasahau kama akimaliza kodi anaweza kupewa notes akaondoka kama wengine waliokuwemo.

Nashindwa kumuelewa huyu mpangaji wetu sijui ulimbukeni au nini?
 
Wakati hajapata nyumba yetu nyeupe alikua mnyenyekevu lakini sasa kawa chui lugha na kauli za kuudhi kila kukicha hapana.
 
Kumbe mlihusika kumpangisha!!!mbona kila anayeulizwa kuhusika huwa anakataa na kusema alimpangisha yule mwingine. Acheni unafiki mliyemtaka mlimsaliti wenyewe
 
Si analipa kodi yenu?
Mnataka kumfundisha na namna ya kuishi?!
Wanajisahau kama mkataba walioingia umempa nguvu kubwa Mpangaji.
Na alisikika akisema kuwa wakimpangisha atawafanya walimie meno kwani ataficha majembe yote mtaani.
 
Kumbe mlihusika kumpangisha!!!mbona kila anayeulizwa kuhusika huwa anakataa na kusema alimpangisha yule mwingine. Acheni unafiki mliyemtaka mlimsaliti wenyewe
Tena walimoangisha kwa gharama kubwa na mbwembwe.Nasikia mpangaji kahariri mkataba na kumpa nafasi ya kuendelea kupanga kwa mwaka mwingine aisee
 
Halafu wanamkana mchana kweupeee tena kwa aibu kubwa
Tena walimoangisha kwa gharama kubwa na mbwembwe.Nasikia mpangaji kahariri mkataba na kumpa nafasi ya kuendelea kupanga kwa mwaka mwingine aisee
 
:) mkataba aliuchukua peke yake msimpangie vya kuishi!!!, vumilieni tu masimango na manyanyaso. maana wakati anatafuta nyumba madalali wake waliwaita majirani MALOFA, wengine waliwasindikiza kwa nyimbo ambazo lait kama wenye nyumba mngekuwa hamjashikiwa akili mngejua maana ya zile nyimbo msinge mpa nyumba. sasa acha ajimwage na kawaambia hataki shobo kwani mkataba alichukua peke yake :)
 
Mpangaji huyo hata mjitahidi kumtoa hatatoka hadi amalize muda anaotaka yeye kuwepo, bora mpokee kodi nyingine kuliko kutopokea na akakaa bure mkataba ujao hahahahaha
 
Samahani mkuu, mkataba wake wa kupangishwa unaisha lini?
Nyumba ipo karibu na pale wanapouzia samaki kule feri?
Nataka nipange nami hapo akiondoka/mkimfukuza.
Napenda sana kukaa ufukweni jamani, duh....
 
Hahah sasa wewe mwenye nyumba unalala kwenye makuti kwa nini asikuzarau
 
Nadhani suluhisho ni kuvunja mkataba tu, ila angalia usalama wako mana jamaa ana bastola kiunoni na ana lindwa na maroboti,...akiwaamuru tu utakiona cha moto.

Ushauri: wochi iti, usifikiri kama unaweza kuvunja mkataba... Noti tu zati eksitenti.
 
Back
Top Bottom