Huyu mwanamke simuelewi nampa matumizi bado analalamika kwa watu

CUBICBOY

JF-Expert Member
Oct 29, 2012
306
223
Habari, wakuu niko kwenye njia panda huyu mwanamke ninayeishi nae simuelewi ni mtu wa kulalamika sana, pesa za matumizi huwa namuachia za kutosha za mwezi mzima lakini amekuwa mlalamishi.

Mpaka kwa watu nimezanae mtoto mmoja sio siri ananipa mawazo kiasi kwamba hata utendaji wangu wa kazi ofisini umepungua msaada wa mawazo tafadhali ninafikiri hatua ya kutaka kumuacha ila nilifikiria mtoto roho inauma sana.
 
Mnaishi pamoja bila ndoa walau inayotambuliwa kiserikali?

Pili, mmeshawahi kukaa mkaongea kuhusu fedha? Mnaishi kama housemates badala ya wanandoa ndiyo maana mnapata shida hamuaminiani kuwa na mazungumzo ya muda mrefu na/au fedha.
 
Kama mnapendana basi ni muda weekend hii mtafuteni mtu akae na mtoto kisha muende sehemu ya utulivu mtakapokuwa wawili tu.

Ongeeni mipango yenu ukimueleza nia yako kwake.

Mnatakiwa mzungumzie fedha ni jinsi gani mtazitumia, ni nini mnapanga kufanya ndani ya mwaka, miaka mitano nk. Je mna akaunti ya mtoto ama mnasubiri akishaanza shule muanze kula mlo mmoja ili asome vizuri? Jinsi mtakavyoamua ni maamuzi yenu ningekushauri kati ya leo mpaka ijumaa u google financial agreements tofauti tofauti za wanandoa.

Mkimaliza hapo, mpange mpango wa kuhalalisha muunganiko wenu itakupa amani unapoacha pesa kidogo hatakuwa na maswali maana anajua mipango mliyonayo na atalalamika tu pale ambapo ataona mipango haitendeki na pesa haipo.

Siku hizi tumerahisisha sana ndoa kuiona haina umuhimu watu wanawekana ndani tu lakini amini nakuambia utaona tofauti kubwa sana mkihalalisha muungano wenu.
 
Kaa nae chini ongea nae akueleze tatizo nini
Mambo mengi nimeshamueleza na anajua kuna kipindi nilipatwa na matatizo ile ulikuwa ngumu nitajaribu kumpa kiasi chote nilichonacho benki, pesa ilipopata kabla ya mwezi anakaanza kutumia mshahara wake lakini ilimuuma sana kiasi kwamba alikuwa akiniona natoka kazini ananuna sana
 
Pamoja na hayo matumizi unayoacha nunua vitu vya jumla mkaa gesi mchele unga mafuta ya kupikia na kila Siku urudi na mfuko wenye kimojawapo kati ya mkate au kitafunwa cha kesho matunda au mboga ya kesho na uwe unampa Pesa nyingine na kumwambia haya ni matumizi yako binafsi muda huo usisahau kulalamika kama hali ya maisha ni ngumu pia haya kama unamwachia kwa wiki msisitizie kama hali ni ngumu unajua hicho kiasi akitoshi wewe unaumia kutafuta na yeye aumie kupanga matumizi
 
Hivi mnaishije?

Mke wako anaongea masuala ya ndoa yenu kwa watu wengine na wewe nae unavurugikaaa mpaka kazi haziendi.:rolleyes::rolleyes:

What happened to the sanctity of marriage? Ama hata ndoa hamjafunga, mnaishi tu pamoja matokeo yake hata mafundisho ya ndoa hakuna mpo mpo tuuu.:eek::eek:

Face her. Be stern. Threaten to withdrawthe amount she is receiving. Just be a man about it!:cool:
 
Mambo mengi nimeshamueleza na anajua kuna kipindi nilipatwa na matatizo ile ulikuwa ngumu nitajaribu kumpa kiasi chote nilichonacho benki, pesa ilipopata kabla ya mwezi anakaanza kutumia mshahara wake lakini ilimuuma sana kiasi kwamba alikuwa akiniona natoka kazin ananuna sana
Duh kama ni hivyo huyo sio mwanamke ni parasite kama hujafunga naye ndoa, mwachie vitu vyote vya nyumbani ukaanze maisha mapya.
 
Kama mnapendana basi ni muda weekend hii mtafuteni mtu akae na mtoto kisha muende sehemu ya utulivu mtakapokuwa wawili tu.

Ongeeni mipango yenu ukimueleza nia yako kwake.

Mnatakiwa mzungumzie fedha ni jinsi gani mtazitumia, ni nini mnapanga kufanya ndani ya mwaka, miaka mitano nk. Je mna akaunti ya mtoto ama mnasubiri akishaanza shule muanze kula mlo mmoja ili asome vizuri? Jinsi mtakavyoamua ni maamuzi yenu ningekushauri kati ya leo mpaka ijumaa u google financial agreements tofauti tofauti za wanandoa.

Mkimaliza hapo, mpange mpango wa kuhalalisha muunganiko wenu itakupa amani unapoacha pesa kidogo hatakuwa na maswali maana anajua mipango mliyonayo na atalalamika tu pale ambapo ataona mipango haitendeki na pesa haipo.

Siku hizi tumerahisisha sana ndoa kuiona haina umuhimu watu wanawekana ndani tu lakini amini nakuambia utaona tofauti kubwa sana mkihalalisha muungano wenu.

Dogo fanya uoe na wewe mwanawane.

I like your maturity these days.
 
Pole sana.

Mtafutie kitu cha kufanya ili nayeye awe anajiingizia kipato au labda wewe hujawa mkweli kuhusu kipato chako anaona unapata hela nyingi lakini unampa kidogo.

Kama mwanamke anakuheshimu na kulea mtoto wako vizuri lakini anaona unampa hela ndogo ya matumizi basi ongea nae kuhusu kipato chako kumuacha sio solution
 
Habari, wakuu niko kwenye njia panda huyu mwanamke ninayeishi nae simuelewi ni mtu wa kulalamika sana, pesa za matumizi huwa namuachia za kutosha za mwezi mzima lakini amekuwa mlalamishi.

Mpaka kwa watu nimezanae mtoto mmoja sio siri ananipa mawazo kiasi kwamba hata utendaji wangu wa kazi ofisini umepungua msaada wa mawazo tafadhali ninafikiri hatua ya kutaka kumuacha ila nilifikiria mtoto roho inauma sana.
Ni Hivi huwa hawatosheki Hawa, ishi nao kwa akili.hela unayompa haimalizi mwezi, na hata ukiongeza haitoshi. Nunua mahitaji Kwa jumla, halafu muachie pesa ya kujiremba na matumizi madogo madogo. Akikushinda mpige chini zari hana mtu Kwa sasa.
 
ukweli unauma, yaani ukizungumza ukweli kuhusu tabia flani flani za kidwanzi, utapoteza marafiki na ndugu, afu kuna watu wanaitwa majirani, sumu sana katika mahusiano ya wasio jielewa
 
Habari, wakuu niko kwenye njia panda huyu mwanamke ninayeishi nae simuelewi ni mtu wa kulalamika sana, pesa za matumizi huwa namuachia za kutosha za mwezi mzima lakini amekuwa mlalamishi.

Mpaka kwa watu nimezanae mtoto mmoja sio siri ananipa mawazo kiasi kwamba hata utendaji wangu wa kazi ofisini umepungua msaada wa mawazo tafadhali ninafikiri hatua ya kutaka kumuacha ila nilifikiria mtoto roho inauma sana.
Mkuu ni kimadaa au Mke wa Ndoa?
 
Back
Top Bottom