Huyu mwanamke si bure, pepo linamsumbua

Huyu mwanamke si bure, pepo linamsumbua

Usimchukulie vibaya kutana nae kisha utamsoma zaidi mbona hata mwanamme unakutana na binti humjui lakini unamtokea na unagonga na pengine anakuwa wife sasa na wewe mwanaume uitwe pepo ?
 
WanaJamvi Habari zenu..
Jaman huu n Mkasa wa kweli ulionitokea Jana. Ilikuwa hivi, nilikuwa kwenye Daladala natoka Tegeta naenda Mlimani City kuangalia muv mpya ya 'Queen of Katwe'.. Kufika Maeneo ya Makongo akapanda Binti Mmoja Mrembo sana.. Mtoto Mashallah.. Alipanda na Kukaa Siti ya Nyuma yangu. Kwa uzuri aliokuwa nao nilitamani ningekaa nae Siti moja ili niweze hata kumsalimia tu.

Basi safari ikaendelea, kufika kituo cha Mpakani(Mbele kidogo ya Mwenge) Kuna Abiria mmoja(mwanaume) alikuwa anashuka, nilipomwangalia vzr nilikuwa namjua.. N mdogo wangu wa Mtaani kwetu.. Akanisalimia halafu akaniomba namba yangu ya Simu.. Nikamtajia(Nilimtajia namba yngu kwa Sauti Kidogo). Kisha yule mdogo wangu akashuka. Namba yangu ya simu iko vzr sio ngumu sana mtu kuikariri.

Mm nilipofika Kituo cha Mlimani City nikashuka. Ile Kushuka tu nikapokea sms, nilipoiangalia ilikuwa namba ngeni.. Sms ilisema 'Nilijua tunaenda wote Mawasiliano kumbe unashukia Mlimani City' nikamuuliza 'Nani Mwenzangu? '. Akanijibu 'Ni yule dada aliyekaa nyuma ya siti yako'... Niliduwaa kidogo huku moyo ukifurahi kupata namba ya yule mrembo.. nikamuuliza 'Umepata wapi namba yangu? '... Akanijibu.. 'Nimeipata wakati unamtajia rafk ako'.. Nikamwambia 'Poa'.

Basi toka Jana mpaka sasa ivi demu ananisumbua kinoma anasema ananipenda sana. Japo nilivutiwa nae lakini kwa jinsi alivyokuwa na ujasiri wa kunifungukia haraka ivi mpka naogopa. Kwa sababu sio kawaida. Hata sisi wanaume ukipata namba ya mwanamke unazuga kidogo hata siku mbili hivi halafu unamtongoza. Lakin kwa huyu demu imekuwa tofauti.. Yan jana kapata namba yngu.. Na jana hiyo hiyo kanifungukia... Wakat hanijui wala nn.. Nikajikuta nawaza kwa sauti 'Mapepo mengi sana Barabarani'. Usikute huyu demu ana Bwana ake.. Halafu barabarani anadandia watu ivi... Mzuka wote kwa huyu demu umeniisha. Yangu n hayo tu jaman
Kabla sijasoma uzi wako,nilijua kabisa utamalizia kwamba demu kaikariri namba yako.basi sawa karibu mjini kijana,ila uwe unatembea na vicks mfukoni,maana kuangalia magorofa shingo itakuwa inakuuma sana.
 
Aisee.
Hizi bahati nyingine sijui kwanini wanapewa wengine
 
Nirushie namba yake mimi naona bahati zikiwaijia mnajifanya mmeokoka eti ana mapepo.
 
Do u believe love at first sight? Usiogope haya mambo yapo na wewe si wa kwanza.
 
Mbuzi kafia kwa muuza karanga...Muuza karanga kamtupa. Rusha namba tukusaidie mkuu
 
Rafiki unavyojiuliza hayo maswali nao Kwa upande wao tukiwatokea wanajiuliza, mfikirie mwenzio
 
Hahahahaaa bro kabla ya ushauri naomba niulize hivi Majini wana blood group gani kama hawana kampime na huyu. Kama vipimo vinaonesha upepo hama jiji, na kama kinasoma poa umepata kiwanja cha kuanzisha nchi yako ya viwanda.
 
Kesho lazima upokee msg yake akidai gas imeisha hapo kwake na anaomba akopeshwe blah, blah......nawaogopa sana wanawake wa Dar
 
Back
Top Bottom