Huyu mwanamke si bure, pepo linamsumbua

Huyu mwanamke si bure, pepo linamsumbua

Tuwaseme

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2014
Posts
645
Reaction score
1,194
Wanajamvi habari zenu,

Jaman huu ni mkasa wa kweli ulionitokea Jana. Ilikuwa hivi, nilikuwa kwenye Daladala natoka Tegeta naenda Mlimani City kuangalia movie mpya ya 'Queen of Katwe' kufika maeneo ya Makongo akapanda binti mmoja mrembo sana. Mtoto Mashallah.. alipanda na kukaa siti ya nyuma yangu. Kwa uzuri aliokuwa nao nilitamani ningekaa nae siti moja ili niweze hata kumsalimia tu.

Basi safari ikaendelea, kufika kituo cha Mpakani (Mbele kidogo ya Mwenge) kuna abiria mmoja (mwanaume) alikuwa anashuka, nilipomwangalia vizuri nilikuwa namjua. Ni mdogo wangu wa Mtaani kwetu. Akanisalimia halafu akaniomba namba yangu ya simu. Nikamtajia (Nilimtajia namba yngu kwa sauti kidogo). Kisha yule mdogo wangu akashuka. Namba yangu ya simu iko vizuri sio ngumu sana mtu kuikariri.

Mimi nilipofika Kituo cha Mlimani City nikashuka. Ile kushuka tu nikapokeaSMS, nilipoiangalia ilikuwa namba ngeni. SMS ilisema 'nilijua tunaenda wote Mawasiliano kumbe unashukia Mlimani City' nikamuuliza 'nani mwenzangu? '. Akanijibu 'ni yule dada aliyekaa nyuma ya siti yako'. Niliduwaa kidogo huku moyo ukifurahi kupata namba ya yule mrembo nikamuuliza 'umepata wapi namba yangu? '...akanijibu.. 'nimeipata wakati unamtajia rafiki yako'.. nikamwambia 'poa'.

Basi toka Jana mpaka sasa hivi msichana ananisumbua kinoma anasema ananipenda sana. Japo nilivutiwa nae lakini kwa jinsi alivyokuwa na ujasiri wa kunifungukia haraka ivi mpka naogopa. Kwa sababu sio kawaida. Hata sisi wanaume ukipata namba ya mwanamke unazuga kidogo hata siku mbili hivi halafu unamtongoza. Lakini kwa huyu msichana imekuwa tofauti. Yani jana kapata namba yngu na jana hiyo hiyo kanifungukia. Wakati hanijui wala nini. Nikajikuta nawaza kwa sauti 'mapepo mengi sana barabarani'. Usikute huyu msichana ana bwana wake, halafu barabarani anadandia watu hivi, mzuka wote kwa huyu msichana umeniisha.

Yangu ni hayo tu jamani.
 
images
 
Kuwen marafik kwanza kwa muda uktazama kama kuna dalil zozote za pepo,kama hazpo PIGAAAAAAAAAAAA ila kumbuka condom
 
...kaka mweke mazingira mazuriii ili uwe una jilia mzigo ki ulainiiiiiiii
 
Back
Top Bottom