Huyu mwanamke ananifaa au niachane nae?

Huyu mwanamke ananifaa au niachane nae?

Habari na ninawasalimia kwa jina la JF,

Kuna msichana nimekuwa nae kwenye mahusiano kwa muda kidogo, lakini kinachonishangaza ni kwamba ikitokea nimesahau simu yangu huwa anaichukua na kuikagua na akikuta kuna namba ya mwanamke hasa wale ambao nimesoma nao huwa tunapenda kutaniana yeye uchukulia kama ni mtu wangu kwahiyo huchukua namba hiyo na kuanza kuwaporomoshea matusi ya nguoni bila hata kuniuliza niko nae vipi.

Baadae hao watu hunipigia simu kuniambia hali hiyo. Mpaka kuna siku moja alinipigia simu dada yangu mida ya jioni na siku hiyo huyu dada nilikuwa nae akaniambia wasichana wako wameanza kiukweli nilikasirika sana kuniambia hivyo. Je, Huu wivu wa kimapenzi mpaka kuwaporomoshea watu matusi ya nguoni au malezi sifuri.

Naomba ushauri wenu.
huo si wivu wa kimapenzi ila ni kukosa busara na adabu....hakuheshimu in short na anataka kukutawala......hio hali idhibiti mapema kama haiwezekan kubadilika achana nae coz mkuu utashindwa kuishi vizuri na jamii inayokuzunguka
 
Back
Top Bottom