Huyu mwanamke ananifaa au niachane nae?

Huyu mwanamke ananifaa au niachane nae?

Na yeye aje hapa aseme sababu ya kuporomosha matusi... Usikute hao wanawake kweli ni wapenzi wako...
 
Matus sidhani kama ni busara hata kama ni kweli
 
Duh! Umeshwahi kufuga mnyama mkali kama ngombe dume lenye pembe, mbwa n.k? Watu dizaini hiyo una wacontrol. Weka pw simu yako au chat na marafiki zako kwa kutumia simu nyingine ambayo haijui... Pia mwambie apunguze wivu...
 
Huyu mwanamke ukimuoa kabla ya kuirekebisha hiyo tabia atatukana hadi wakwe.Japo wivu ni kitu cha kawaida but kupekua simu ya mwenzi wako ni dalili za kutoheshimiana.Mrekebishe awe mstaarabu na kama una tabia za kutaniana na wanawake hovyo acha.Kukupenda anakupenda kweli ila mjengee mazingira ya kukuheshimu ,kuwa muwazi kwake ajue jisi gani unakerwa na hiyo tabia.Akishindwa kubadilika tafuta mwingine mapema.Ndoa za wanawake wa hivi ni majipu sugu.
 
Habari na ninawasalimia kwa jina la JF,

Kuna msichana nimekuwa nae kwenye mahusiano kwa muda kidogo, lakini kinachonishangaza ni kwamba ikitokea nimesahau simu yangu huwa anaichukua na kuikagua na akikuta kuna namba ya mwanamke hasa wale ambao nimesoma nao huwa tunapenda kutaniana yeye uchukulia kama ni mtu wangu kwahiyo huchukua namba hiyo na kuanza kuwaporomoshea matusi ya nguoni bila hata kuniuliza niko nae vipi.

Baadae hao watu hunipigia simu kuniambia hali hiyo. Mpaka kuna siku moja alinipigia simu dada yangu mida ya jioni na siku hiyo huyu dada nilikuwa nae akaniambia wasichana wako wameanza kiukweli nilikasirika sana kuniambia hivyo. Je, Huu wivu wa kimapenzi mpaka kuwaporomoshea watu matusi ya nguoni au malezi sifuri.

Naomba ushauri wenu.
"Ndo matokeo ya kutembea na watoto wa shule haya"
 
Ila kuna watu wana mioyo, nitukane watu kisa boyfriend asyeeeeeeeeeeee. Yeye adeal na anayemuhusu,
 
Mazoea yapi ndugu
Mazoea ya huyo msichana wako kupekua siku yako, pia mazoea ya wewe kuchat na wanawake, sitaki ni marafiki ila punguza kidogo.

Pia huyo binti sio mstaarabu hawezi kumtukana mtu from no where.
 
Bro, kila jambo hujipimia mwenyewe kwa uzito fulani. Maisha ya mapenzi siku zote ni lazima mmoja anapenda zaidi.

Tambua thamani ya mapenzi yake kwako kwanza. Naye aweze kujua unamthamini. Kwa kufanya hivyo unamjenga kisaikolojia kama anahitajika ktk maisha yako na kuaminiana.

Kisha baada ya zoezi Hilo kukamilika, muwe na tabia ya kuelezana vitu gani mnapenda na msivyovipenda.

Linda mahusiano yako brother ikiwa mnapendana. LOVE IS HARD TO FIND..
 
Back
Top Bottom