Twende kwenye Mada bila kuwachosha...
Sehemu ninayofanyia kazi kuna Dada mmoja rafiki yangu sana,huwa tunataniana na tunaukaribu ule wa kirafiki,huwa tunashauriana baadhi ya mambo na tunafanya kazi kwa ukaribu sana kutokana na ukaribu wa vitengo vyetu.Hayo pamoja na mengine yamenifanya Mimi kuwa karibu nae sana kuliko MTU mwingine yeyote pale ofisini.
Ofisini kwetu tunafanya kazi na wazungu kadhaa ,ni kwa muda sasa amekuwa akiniomba ushauri juu ya mzungu mmoja ambae amekuwa akimtongoza Mara kwa mara. Kwaninavyomjua nilijua kabisa kwamba hawezi kumkubalia kwani alinieleza zaidi ya Mara moja jinsi gani asivyovutiwa na ngozi nyeupe...anadai huwa anaskia kichefuchefu na hawapendi kweli kweli....
Juzi kati huyo mzungu bwana alinifuata na kunitia ktk majaribu,alinieleza ni jinsi gani anampenda yule binti na yupo tayari kumuoa endapo atakubali kuwa nae.
Kiukweli mzungu yupo vizuri financially na ameahidi kumsaidia sana huyo mke wake mtarajiwa endapo atamkubalia kuwa nae....amenieleza plani nyingi nzuri ambazo hajazi expose kwa binti .
Amenifuata kuniomba nimsaidie kumpata huyu binti kutokana naukaribu tuliokuwa nao...
Anataka huyo Dada ampende bila kutumia ushawishi wa pesa..
Nimejaribu kuongea Mara kadhaa na huyu Dada amekataa kabisa kuwa na mahusiano na hiyo ngozi nyeupe,.
Nimetumia kila mbinu kushawishi lakini amekataa kata kata..Isitoshe hayupo kwenye mahusiano na MTU yeyote kwa sasa.
Sipendi ngozi nyeupe......
Naomba ieleweke kwamba Mimi sio kuwadi,kutokana na circumstances iliyopo nililazika kutoa msaada,lengo langu Dada huyu awe na maisha mazuri na mzungu spate kipendacho roho..Ukizingatia huyu Dada anatoka ktk familia duni huku ndugu na wadogo zake wakimtegemea pamoja na kwamba ana pesa kidogo za kubadilisha mboga.
Nimeleta kwenu wajuvi wa mambo JF mtoe ushauri nini kifanyike.
Asanteni.