Huyu mwanamke anamsimamo mkali au?

Huyu mwanamke anamsimamo mkali au?

audacious

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2012
Posts
240
Reaction score
397
Twende kwenye mada bila kuwachosha,

Sehemu ninayofanyia kazi kuna dada mmoja rafiki yangu sana, huwa tunataniana na tunaukaribu ule wa kirafiki, huwa tunashauriana baadhi ya mambo na tunafanya kazi kwa ukaribu sana kutokana na ukaribu wa vitengo vyetu. Hayo pamoja na mengine yamenifanya mimi kuwa karibu nae sana kuliko mtu mwingine yeyote pale ofisini.

Ofisini kwetu tunafanya kazi na wazungu kadhaa ni kwa muda sasa amekuwa akiniomba ushauri juu ya mzungu mmoja ambae amekuwa akimtongoza Mara kwa mara. Kwani navyomjua nilijua kabisa kwamba hawezi kumkubalia kwani alinieleza zaidi ya Mara moja jinsi gani asivyovutiwa na ngozi nyeupe anadai huwa anasikia kichefuchefu na hawapendi kweli kweli.

Juzi kati huyo mzungu bwana alinifuata na kunitia ktk majaribu, alinieleza ni jinsi gani anampenda yule binti na yupo tayari kumuoa endapo atakubali kuwa nae.

Kiukweli mzungu yupo vizuri financially na ameahidi kumsaidia sana huyo mke wake mtarajiwa endapo atamkubalia kuwa nae amenieleza plani nyingi nzuri ambazo hajazi expose kwa binti.

Amenifuata kuniomba nimsaidie kumpata huyu binti kutokana na ukaribu tuliokuwa nao.

Anataka huyo dada ampende bila kutumia ushawishi wa pesa..

Nimejaribu kuongea Mara kadhaa na huyu dada amekataa kabisa kuwa na mahusiano na hiyo ngozi nyeupe,.

Nimetumia kila mbinu kushawishi lakini amekataa kata kata..Isitoshe hayupo kwenye mahusiano na mtu yeyote kwa sasa.

Sipendi ngozi nyeupe......

Naomba ieleweke kwamba mimi sio kuwadi, kutokana na circumstances iliyopo nililazika kutoa msaada,lengo langu dada huyu awe na maisha mazuri na mzungu spate kipendacho roho.

Ukizingatia huyu dada anatoka ktk familia duni huku ndugu na wadogo zake wakimtegemea pamoja na kwamba ana pesa kidogo za kubadilisha mboga.

Nimeleta kwenu wajuvi wa mambo JF mtoe ushauri nini kifanyike.

Asanteni.
 
Kuna mawili hapa nayaona......

Kwanza namsifu na kumpongeza sana dada, kuolewa kwa sababu ni mzungu au ana hela ni kujaribu kujitafutia majaribu na shida huko mbele, muache dada aolewe na anaempenda. Ingekuwa ni wewe mkuu unaombwa au kushawishiwa kumuoa mtu fulani usiyempenda kabisa hadi kufikia hatua unasikia kichefuchefu ukiwa nae ungekubali kwa sababu fulani yoyote ile kama ya uwezo au yoyote ile?

Pili, huyo mzungu nae vipi? Anaingiaje na gia za kusema akinikubali nitamsaidia sana? Tongoza gani hiyo? Ni bora angeng'ang'ania tu kuwa anampenda baaaasi! Hayo ya kumsaidia yangekuja yenyewe automatic mbeleni huko.

All in all, namsifu dada na usimlazimishe wala kutumia ushawishi kumuingiza kwenye ndoa na asiyempenda. NDOA NI ZAIDI YA KUVAA SHELA NA SUTI MKUU!
 
Huyo mzungu kuwa na pesa haimaanishi huyo dada ajirahisi kwa kuwa hali yake duni!Mapenzi ni zaidi ya pesa,mapenzi ni hisia,mapenz hayalazimishwi.Muache huyo dada na msimamo wake kwakuwa anajielewa na anajua anahitaji nn ktk maisha yake!
 
Mwambie aache ubaguzi wa rangi, kila siku ubaguzi unapingwa yeye asikii?? Huyo anataka maumivu ya milele, kuna wazungu waaminifu sana ila hakuna mwafrica mwaminifu, atajutia when it's too late. Kuna watu wamebadilika maisha yao kuanzia amani ya nafsi hadi kiuchumi ktokana na kuwa na mahusiano na wazungu,
 
Kuna rafiki angu wa kike alikuwaa hapendii wakaka weusiiu...yaniii hata huyo mkaka ampee nini hana hata ilee kumfikiriaa so ni kipendacho rohoo... mzungu huyo anataka kumuoa sasa hapo dada hampendi na hana furaha naee boraa ingekuwa kiselaa... dada asimamiee msimamo wakee kwa ajili ya furaha yake maana Furaha na Amani ya moyoo ni boraa zaidi kuliko fedhaa
 
Kuna mawili hapa nayaona......

Kwanza namsifu na kumpongeza sana dada, kuolewa kwa sababu ni mzungu au ana hela ni kujaribu kujitafutia majaribu na shida huko mbele, muache dada aolewe na anaempenda. Ingekuwa ni wewe mkuu unaombwa au kushawishiwa kumuoa mtu fulani usiyempenda kabisa hadi kufikia hatua unasikia kichefuchefu ukiwa nae ungekubali kwa sababu fulani yoyote ile kama ya uwezo au yoyote ile?

Pili, huyo mzungu nae vipi? Anaingiaje na gia za kusema akinikubali nitamsaidia sana? Tongoza gani hiyo? Ni bora angeng'ang'ania tu kuwa anampenda baaaasi! Hayo ya kumsaidia yangekuja yenyewe automatic mbeleni huko.

All in all, namsifu dada na usimlazimishe wala kutumia ushawishi kumuingiza kwenye ndoa na asiyempenda. NDOA NI ZAIDI YA KUVAA SHELA NA SUTI MKUU!
Nenos kuntule sana
 
Back
Top Bottom