The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,950
- 12,550
Habar wana jf
Bila kupoteza muda, nimewahi kuingia kwenye mgogoro na aliyekuwa mkuu wa mkoa x kipindi cha serikali ya awamu ya NNE ya JK.
Huyu mkuu amewahi kumuamrisha mkurugenzi wa Halmashauri ambayo nilikuwa naifanyia kazi kuwa nimekula fedha za mradi fulani ndani ya Halmashauri hiyo,
Nilisimamishwa kazi na maslahi yangu pia yalisimamishwa, kupisha uchunguzi, mwaka mzima nachunguzwa bila majibu sahihi, na ukumbuke mwaka mzima huo sipati mshahara wala posho, familia yangu ikatabika ile mbaya, watoto wakashindwa kusoma
Baada ya mwaka huo kuisha, wakaguzi wakaja na majibu kwamba sijakula hata senti moja ya mradi
Mwaka 2016 nikarudishwa kazini ila nikaomba kuhamishwa kwenda Halmashauri nyingine mkoa mwingine
Katika mabadiliko ya wakuu wa mikoa na wilaya yaliyofanywa na JPM, huyo mkuu wa mkoa kapigwa chini na Halmashauri niliyopo ndo anayokaa anafanya business zake
Sasa kuna zabuni imetolewa hapa Halmashauri na kuna maombi mbalimbali yanaletwa kwa ajili ya mradi huo
Huyu ambaye alikuwa mkuu wa mkoa naye ameomba mradi lakini hana sifa ya kupewa mradi, hakidhi vigezo vya kupewa mradi ila anapigiwa pande na mwenyekiti wa Halmashauri ananishawishi tumpe mradi. Cha kushangaza na yeye bila aibu ananipigia sim tumpe kipao mbele
Sasa nakaa nawaza hivi huyu mkuu anajua kuwa amewahi kuniachisha kazi kwa tuhuma ambazo si za kweli ,au amesahau au hanijui?
Mbona ananipigia simu na kuongea na mimi friendly sana?
Sasa najiuliza, nimpinge asipewe mradi maana hana sifa, au tumpe tu halafu nimkumbushe hicho kisa ambacho amewahi kunifanyia, au nifanyeje wakuu
1. Usiishi kwa visasi. Mpende adui yako, msamehe. Amani ya nafsi yako ni muhimu zaidi kuliko jambo lolote. Amani ipo ktk nguvu ya msamaha. Bila kusamehe na kusahau, utateseka maisha yako yote.
Kumbuka kuwa kila linalotukokea katika maisha yetu, Mungu huwa anataka atufundishe jambo fulani. Na fundisho hilo liko wazi sasa usoni mwako..
Kwamba, siku zote maisha ni mlima. Kuna kupanda na kushuka. Na pia usimtendee binadamu mwenzio ubaya kama ambavyo wewe hupendi kutendewa. Mpende jirani yako kama kama unavyoipenda nafsi yako !!
Hili ndilo fundisho tunalolipata kupitia mkasa huu na ndugu huyu !!
Ndiyo maana maandiko matakatifu (Neno la Mungu) yanatuambia, furahini siku zote iwe nyakati za taabu na mateso na kukosewa ama zile za ujazo wa kila kitu.
Na pia yanaendelea kutuambia, tunapokosewa tunapaswa kusamehe hata saba mara sabini. Msamehe na endelea na maisha yako, hutapungukiwa na kitu chochote.
2. Kwa upande wa zabuni aliyoiomba, tenda haki kwa mujibu wa sheria na vigezo/masharti ya zabuni hiyo. Usiingie ktk mtego wa "rushwa ya usaidizi ama upendeleo"
Aidha, binafsi naamini kuwa, uamuzi wa kutoa tenda ama zabuni kwa mzabuni yeyote hayatolewi ama hautolewi na mtu mmoja. Naamini ipo kamati/bodi ya zabuni katika halmashauri hiyo.
Kwa maana si wewe peke yako unayeamua nani apewe na nani asipewe. Zaidi sana kama nilivyosema hapo juu, kuwa, unaongozwa/mnaongozwa na sheria na kanuni/vigezo vya kumpa zabuni mtu yeyote.
Zinagatia/zingatieni hilo..
Kama anakidhi vigezo vya zabuni na kuwashinda wenzake, apewe bila kujali ubaya aliokutendea.
Kama hakidhi, atatupwa na vigezo ama sifa na yakupasa umwambie waziwazi kuhusu hilo ili atakapokosa zabuni, asije kudhani wewe ndiye umemfanya akose !!
Usiku mwema, Mungu akubariki.