M.E.M.A
JF-Expert Member
- Jul 27, 2013
- 1,373
- 472
Habari za wakati huu wana MMU.
Kuna bibie mmoja nilimtokea kama wiki mbili hivi zilizopita. Kwa kweli ni mzuri sana..wa umbo (mengineyo sijui). Nilitaka kuona kama lile jini MAKATALIWA bado linanisumbua. Bahati nzuri akakubali...(nilishangilia sana moyoni).
Tatizo na habari iliyonileta hapa ni kwamba simuelewi. Nikimuita tupange mambo yetu anakuja ndani ya dakika mbili anasema anawahi nyumbani kupika (nimechunguza sio house girl). Nyumbani kwangu ameshafika mara mbili. Angalau weekend hii alikaa kwa lisaa limoja na hata kuondoka kwake ilikuwa hoja ile ile (nawahi kupika). Nikimpigia simu na kumbusu zile za kisimu simu harudishi..anasema kuna watu. Ukimtumia ujumbe wa maneno anajibu short short tu (k, poa, sawa, asante, hahaha)... basi nikaona isiwe tabu na mimi niache kujifanya nilielewa sana somo la kutunga sentensi, na mimi nikaanza kujibu hivyo hivyo...tena nikayafupisha zaidi (k, asnt, mh,). Baada ya hayo kaanza kunilalamikia simjali, namjibu kifupi kifupi kama vile sitaki, simbusu kwenye simu...😕
Kwa kweli sielewi nifanyeje. Na sio mtoto huyu miaka 25 sasa.