Mpeleke kwa daktari bingwa wa watoto (Dr Masawe) atakusaidia sana. Yule babu ni bingwa wa ukweli--kuna mtoto wangu alishindikana kwa madaktari wote Tanzania nzima, lakini nilipomfikisha kwa huyu babu, akatibiwa na kupona faster. Ila itakupasa uende ufanye appointment naye kwa kuwa ana-attend wagonjwa 10 tu kwa siku na utapaswa kudamka kuwahi sana ili uwahi namba. Hospitali ya Dr Masawe ipo karibu na makao makuu ya Airtel kwenye makutano ya barabara ya Ali Hasan Mwinyi na ile barabara inayotokea kinondoni kwa Manyanya (nimeshanu jina la barabara). Hospitali inaitwa Furaha Medical Centre. Ukifika maeneo hayo ya Airtel headquaters utaiona. Pole kwa kuuguza, Mungu atamponyesha huyo malaika.