Huyu kwa Kiswahili anaitwaje?

Huyu kwa Kiswahili anaitwaje?

Huyu ni DUMA. Kuna Chui, Duma na Chita wote wote ukiwaangalia kwa haraka wanafanana na kwa mtu ambaye hawajui vzuri anaweza kushindwa kuwatofautisha na kuwaita Chui.

Chita ndo PUMA??
 
Tiger ni jinale kwa kiingereza,
Kiswahili chake ni "Simba-Marara". Marara ni ile milia yake inavyoonekana. Ana nguvu na speed kuliko simba wa kawaida. Pia ana uwezo wa kulifuata windo lake ndani ya maji.

Wanaosema ni Duma wamekosea, maana duma anaitwa Cheetah
kwa kimombo

Tafsiri hii niliipata zamani kidogo (miaka ya 80 mwishoni) wakati nasoma picture-book ya wanyama.

Hapo kwenye red nafikiri ulimaanisha CHEETAH
 
  • Thanks
Reactions: Paw
4_big-cats.jpg

Huyu kwa jina la kimombo anaitwa Tiger sina uhakika ila nahisi kiswahili chake pia huitwa Dubu, sio Duma maana Duma ni Cheater kimomb.

Mkuu Heshima mbele,
Hapo umeteleza kidogo Dubu kwa kikoloni ni Bear na pisha zake hizo
Bear(1).jpg

bear_grass.jpg

Hao ni bear grass na huyu chini ni Polar bear
polar bear watching and ecotourism.jpg
 
Huyu ni DUMA. Kuna Chui, Duma na Chita wote wote ukiwaangalia kwa haraka wanafanana na kwa mtu ambaye hawajui vzuri anaweza kushindwa kuwatofautisha na kuwaita Chui.

hata wewe huwajui vizuri Duma=Cheetah, hapa ni kama umemchora Messi kwenye majibu ya pepa.
 
Hata nami lilinijia jina hili. Sijui ni kwanini walimuita "Simba Marara", km alivyoandika Paw hapo juu. Ni bora basi wangemuita "Chui Marara".

Tofauti hizi zinaletwa na makabila mbali mbali yanavyoathiriwa na lugha zao katika kutowa maana ya kitu kimoja. Kwa mfano neno marara linakaribia na kitu kilichochanika chanika wakati wengine mpangilio unaoonekana wanauona kama ni miraba.
 
Duh hatari

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Sio cheater. Ni cheetah. Tukishirikiana tutaijenga nchi pamoja.

Usishangae sana, inaposemwa elimu yetu imeshuka tafsiri yake ni hiyo. Utakuta huyu ni degree holder na ameshindwa kutofautisha kati:-

-Cheetah ambaye ni Duma, (Cheater ni mtu asiye mwaminifu katika mahusiano, mzinzi au mwasherati)
-Dubu ni Bear
-Chui ni Leopard
 
Huyu ni DUMA. Kuna Chui, Duma na Chita wote wote ukiwaangalia kwa haraka wanafanana na kwa mtu ambaye hawajui vzuri anaweza kushindwa kuwatofautisha na kuwaita Chui.


DUMA na CHITA ni tofauti mkuu!!?..............hapa umekosea.kinachoonekana kwenye picha ni tiger mkuu.duma ni kiswahili na kikoloni anaitwa cheetah.ana mistari miwili myeusi toka machoni mpaka midomoni kwa pembeni.hana nguvu na mbinu nyingi za kuwinda hivyo silaha yake kubwa ni mbio..the thing can run bana,wacha mchezo!

leopard ana madoa au labda uyaite mabaka.........muwindaji mzuri,mkorofi sana,si mzito sana (yaani ana nguvu kiasi) na mbio pia,japo si kama duma.

tiger ni mkubwa kulinganisha na hawa paka wote isipokua simba.hivyo ni mzito zaidi pia,hana mbio sana(japo huwezi shindana nae kwakweli..lol!),ana maguvu mengi mno kwasababu hiyo.wanasema kwakuwa hawezi kimbia sana,hivyo ana mbinu kali zaidi za uwindaji kulinganisha na hawa wengine(kutoa simba).ni mtulivu sana anapowinda.ana milia/mistari ya kushuka mpaka tumboni.rangi nyeupe,nyeusi na dhahabu....binafsi napenda sana rangi zake kwakweli!ana fanana na paka pori japo paka ni wadogo sana kulinganisha na huyu,japo pia si wadogo kama paka wa kufugwa na ni hatari mno hawa paka.


hicho ndo kidogo nikijuacho kuhusu hawa ''jamaa''....naamini sijakupotosha mkuu.
 
4_big-cats.jpg

Huyu kwa jina la kimombo anaitwa Tiger sina uhakika ila nahisi kiswahili chake pia huitwa Dubu, sio Duma maana Duma ni Cheater kimomb.

DUBU ni BEAR mkuu, nadhani hilo la simba mirara ni lenyewe zaidi.
 
Leopard(chui) na Cheetah(duma) huwa wanapatikana Africa hususan Afrika mashariki ikiwamo Tz.Huyo mnyama uliyemuonyesha(Tiger) anapatikana ASIA na hapatikani sehemu yeyote Africa, kwa hivyo basi hatokua na jina la kiswahili.Huyo mnyama kwa Kihindi anaitwa PAKA na kwa Kitamil (Sri lanka)anaitwa PULLI
 
Nimesoma maoni yate humu na nimegundua kuwa wengi wetu bado tuna uelewa mdogo mno katika mambo ya wanyama pori,huyu mnyama hata mimi nilikuwa silijui jina lake lakini thanks Paw kwa maelezo mazuri.Ila walionichekesha zaidi ni wale walioamua mpaka kuelezea tabia zake wakati ni uongo mtupu ulioelezewa hahahahahahaha...
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: Paw
Back
Top Bottom