Mume kwa mkabala huo huamini kwamba anazo haki zote kwa mwili wa mkewe na mkewe hana haki hizo. Mke naye huamini kwamba, msemaji wa mwisho juu ya mwili wake ni mume.
Bila shaka utakubaliana na mimi kwamba, kauli kama vile, mke ni pambo la nyumba, hazijitokezi tu kwenye jamii.
Kwa kuwa mwili wa mke ni mali ya mume kwa kila hali na jamii imetufundisha kwamba, jukumu la mke ni kumstarehesha mume na kumzaliwa watoto, na hii starehe pamoja na watoto vimejifunga kwenye tendo la ndoa. Mwenye haki ya tendo la ndoa kionevu na kifedhuli huwa ni mume.