Nkenangere
Senior Member
- Mar 22, 2019
- 174
- 101
Bigteacher unaacha kuitendea haki fani yako badala yake unafanya mzaha na jambo hili.Kwahiyo mita mia karibu ee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Najashuhudia adha ya suala hili walahalikugusi. Ilielezwa kuwa mradi wa REA wa kusambaza umeme vijijini ungewawezesha "wanyonge" kupata umeme kwa gharama nafuu. Inakuwaje mazao na mimea mingine ya wananchi inafyekwa bila fidia alafu wasisambaziwe umeme ilhali nguzo zimesimikwa kwenye compound zao?
Kwa hili wakandarasi ambao hawakusimamiwa vizuri ilikuwa profit maximization in collusion na wasimamizi kwa gharma za walengwa. Jukumu la REA ni kutoa fedha. TANESCO wao wanasimamia. Pengine hawakupa wakandarasi viwango na vigezo walivyopaswa kufuata kutumiwa kuwakagua. Matokeo yake yakoje? Serikali imepata hasara kubwa:
1. Transforma nyingi zinalipuka (blow),
2. Nguzo za umeme huanguka na kukosesha waliobahatika kupata kukosa nishati,
3. Zoezi la kuunganisha umeme linaonekana kufanywa kibaguzi, na
4. Lengo la kufikisha umeme vijijini kwa gharama nafuu halitimii.