buzitata
JF-Expert Member
- Apr 11, 2017
- 2,007
- 7,118
habarini wana jamvi
siku moja katika pita pita zangu nlikutana na tukio ambalo ilibaki kidogo linitoe machozi
ukiwa pale maeneo ya kariakoo (dar es salaam) katika stend za magari yaendayo temeke na gongolamboto (imepakana na kituo cha mwendo kasi)
ukishuka tu kwenye gari utakutana na ombaomba wengi, wengine wamejifunga bandage wengine wanamagongo ya kutembelea ila achana na hao wote kuna mlemavu mmoja yeye anaulemavu wa miguu pamoja na mikono
chakushangaza badala ya kuomba omba kama wenzie yeye amenunua mzani wa kupimia uzito na anapimisha watu kwa shillingi mia mbili tu
nikaja kujitathmini na mimi je ningekua na ulemavu kama yeye ningeweza kuyafanya hayo(kujitaftia riziki bila kuomba omba?)
lengo la kuanzisha huu uzi ni kuwaomba wenzangu kama mnamioyo mikunjufu juu ya hawa wajasiliamali ambao wana ulemavu tuwe tunawapa vipaumbele ili waweze kujikwamua kimaisha
sio lazima upime uzito kwa shilingi mia mbili bali unaweza hata kumzidishia kidogo kwasababu hawa watu wanapitia mengi kwanza wengi wao wanakuwa ni wagonjwa na hufanya hivyo ili kujipatia pesa za kuenda kupatiwa matibabu........
tafadhalini sana wanajf kama unapata muda pitia pale kariakoo stend ya temeke mchangie hata shilingi mia na mungu atakuona tuachane na hawa wanaokodi watoto ili kuifanya kazi ya kuomba omba iwe rahisi kwao kupewa pesa kwa kuonewa huruma
kuna walemavu wakiwezeshwa wanaweza kinachotakiwa ni kuwawezesha tu jamani
sio lazima kila anayezaliwa na ulemavu basi aishi katika umaskini
tukiamua kuamsha furaha za wanyonge inawezekana sio lazima mpaka awe omba omba
KARIBUNI na wewe utoe lako ulilowahi kulishuhudia na kukustaajabisha
kisha gonga like hapo