Huyu jambaa mzima kweli

IamError_D

JF-Expert Member
Dec 21, 2011
427
225
Nilienda kikazi Singida. Asbh
mapema sna mm niko Ubungo
nikapata tiketi ya dirishani. Muda
kidogo akaja Jamaa kakaa pembeni
yangu mm nikajua niko nae seat
moja. Sasa mshangao ndo
uliponianza:
Jamaa kaweka begi akatoa maji
makubwa na keki mbili akala.
Sikushangaa. Kufika Chalinze
kanunua Mayai ya kuchemsha 3 na
Hindi 1 la kuchemsha na Soda ya
kopo (Fanta) akapiga taratiiibu!!
Kufika Msamvu!! Kashuka karudi na
Chipsi Mayai kanikuta nimekaa
kwenye seat maana sikushuka. Gari
halijaondoka kaita muuza korosho
kanunua pakti kubwa huku
kachukua machungwa 4. Mimi
nikaanza kua na mashaka aisee!!
Jamaa kapiga Taratibu!!
Tumeingia Dodoma saa saba hivi
Heee!! Pale Four Ways watu
tunashuka mchana tukafinye maana
njaa sasa ilikua inauma Jamaa nae
kashuka nikaguna MHH!!! Lahaula!!
Jamaa kaingia Hotelini nae kaagiza
Wali Samaki na Coca cola. Kwa kweli
mimi nikaanza kumuogopa yule
Jamaa!!! Nikaanza kufikiria mbona
haombi kuchimba dawa?
Muda umefika gari linaondoka
nikajua Jamaa lazima ataomba
kuchimba dawa!! Lazima akakate
GOGO!! Mhh!! Jamaa kainuka kavuta
begi lake kapekua pekua karudisha
kukaa namuona kashika Pande la
muogo wa kuchoma na maji ya
Kilimanjaro makubwa!! Kwenye
mfuko wa shati kuna biskuti za
chokleti. Nikainuka mbio mpaka kwa
Dereva.
Niliogopa AISEE!!
Nikasema
"HIVI HUYU AKIJAMBA HUMU
NDANI ITAKUAJE?"
 
Top Bottom