Huyu jamaa ni shujaa wa wapi

hazole1

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2015
Posts
4,319
Reaction score
3,919


Duniani mtu haitakiwi ujiulize utafia wapi. ila cha msingi inabidi ujiulize siku ukifa utakumbukwaje.

Leo ktk pita pita zangu nimekutana na hiyo picha na nimependa jinsi alivyo kumbukwa na nikataka kumjua kiundani zaidi huyo shujaa ni nani.
 
...huyo jamaa ni wa South Africa,..aligoma kuwapigia magoti makaburu _wakamuua na alikata roho huku akisisitiza watu wapambane mpaka tone la mwisho dhidi ya udhalimu wa makaburu
 
...huyo jamaa ni wa South Africa,..aligoma kuwapigia magoti makaburu _wakamuua na alikata roho huku akisisitiza watu wapambane mpaka tone la mwisho dhidi ya udhalimu wa makaburu
Huyo jamaa alifanya vizuri sana.
 
Huyu ni shujaa wa CHADEMA
 
Huyo ni Solomon mahlangu mpigania uhuru wa South Africa anakumbukwa kama mpigania uhuru mdogo sana na aliyejitoa kwa hali na mali aligoma kuwatetemekea makabulu na kuuwaw kwa kunyogwa hadi kufa akiwa na umri wa miaka 23 tu mwaka 1976. ..ujumbe aliyoutoa kabla ya kufa kupitia mama yake ni huu.

‘My blood will nourish the tree that will bear the fruits of freedom. Tell my people that I love them. They must continue the fight.’ - Solomon Kalushi Mahlangu

Ktk kumuenzi sisi tanzania kuna kampasi ya wasouth Africa kule morogoro mazimbu ilipewa jina la solomoni (kampasi ndogo ya chuo cha sua pia) na shule ya msingi moja nzuri sana sijui sahivi kama bado ipo.
 
Asante mkuu

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…