Tafuteni mshauri nasaha aje hapo home kwenu aonane nae, kukubaliana na tatizo ni hatua kubwa sana ya kukabiliana na tatizo afu jaribun kumwelewesha kuwa huo sio mwisho wa maisha, na kitu kikubwa ambacho wengi huwa hawakijui ni kwamba ukianza kutumia dawa za ARV kwa usahihi unakuwa huna uwezo wa kumwambukiza mtu mwingine ndo mana HIV activists wanashaur watu wapime kujua afya zao na kama wameathirika basi CD4 count zikifika level flan wanatakiwa waanze dozi manake in the longrun tunaweza tukatokomeza hili gonjwa kwa style hiyo, mkuu yafanyie kazi haya nloshauri, ukishindwa rudi tena nikupe njia mbadala.