Huyu hapa mbaya wako

Huyu hapa mbaya wako

Mbaya wako Ni mbaya wako tu hawezi hata siku moja kuwa mpenzi wako,ndugu yako au Raifiki yako haiwezekani

Huyo sio mpenzi wako, ndugu yako Wala Raifiki yako Ni mbaya Wako full stop
 
Hapo vipi..??

Mweka mada amekandia watu wanaotuzunguka na kusahau kuwa wewe mwenyewe unaweza kuwa mbaya wa maisha yako!!..

Kama akili haitoshelezi unafikiri nani atakaepata athari wa kwanza kwa akili hiyo..??

Kama utaendekeza uvivu,ujinga,ushetani na kila aina ya upuuzi hapo hauhitaji mtu mwengine awe adui wa maisha yako!.. isipokuwa wewe mwenyewe umeshakuwa adui wa maisha yako binafsi.

Kwangu mmbaya wangu wakwanza ni Mimi mwenyewe!!… Kabla haujashuku wenzio je wewe umejishuku..??
Kabla hujasema wenzio kuwa wananuka je,wewe umejihakiki haunuki..??

Ikiwa tutaweza kujisimamia uimara wa nafasi zetu basi hatutaona nani mbaya!.. nafasi ya kwanza ya ubaya kujishuku ianze nawe ya pili ije kwa wengine ila ujihakiki kuwa nawe huna ubaya..

Maisha sometimes hayanaga formula!.. haka ka kauli kapana!.. siku njema.
Kaka hauwezi kuishi kwakujishuku au kujihofia kuwa wewe ni mbaya wa maisha yako na badala yake maisha yako hayatokwenda vilivyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom