Huyu hapa mbaya wako

Huyu hapa mbaya wako

Joined
May 29, 2020
Posts
30
Reaction score
24
HUYU HAPA MBAYA WAKO[emoji116]
Kabla ya yote ivi unamjua mbaya wako? Hapana ndiyo jibu lako la haraka haraka. Sasa kama haumjui mbaya wako hebu wacha nikujuze ili na wewe upate kumfahamu na ujue jinsi ya kumuepuka ili asikudhuru kwa namna yeyote ile.

1) NDUGU YAKO
Huwezi kuamini ndugu yako ambaye unamuamini sana unampenda sana kuliko wote huyo ndiye mbaya wako sijaongea kwa ubaya ila nakupa ufanisi wa kufanya uchunguzi.

2) RAFIKI YAKO WA KARIBU
kaka zangu dada zangu naombeni niwaambie mbaya wako ni yule rafiki yako unayemshirikisha vitu vyako vingi sana huyo ndiye anaye didimiza hali ya maisha yako na ndiye anayekupa wakati mgumu unaoupitia kwa sasa.

Sijasema kwa nia mbaya wala sihitaji mgombane ila ni ukweli na siri nimekupa swali langu kwako je' unauwezo wa kumjua mbaya wako bila yeye kujua kama umemjua? Hilo haliwezekani kwa baadhi ya watu.

3) MPENZI WAKO
jamani jamani huwezi kuamini mpenzi uliyenae ndiye anaekufitini sana kwasababu hakupendi na wala sio chaguo lako huwenda kapenda pesa zako hajakupenda wewe au kaoenda tako lako na jicho lako hivyo akitisheka ataanza kukufanyia visa vya chinichini au juu juu ili kukuharibu kukuharibia au kukupoteza kabisa. Ila sijasema muachane samahanini huu ni ukweli tuu ninaouongea leo ili uchukue hatua.

Jinsi ya kuepukana na watu wa aina hii ni hivi:
1) hebu kuwa bize kufanya mambo yako.

2) uUipende mahusiano yeyote bila uchunguzi wa kina

3) Usimshirikishe mtu mambo yako yanayohusu mafanikio yako au siri zako

4) Umakini unahitajika bila kushau mfumo wa IQ ndiyo utakupa muongozo mzuri wa maisha yako.

Sibahatishagi maneno yangu ni ya ukweli na nimechunguza kwa kina ndipo nimekushirikisha na wewe ndugu msomaji kama unaswali au ushauri niandikie hapo chini nitapitia.

Habari hii imeandikwa na mwandishi wako:mfalme wa wafalme.

enemy.0.jpg
 
Inategemeana mkuu sio wote wengne wana wapenzi wao na wamekuwa muhimu zaidi na wamewasidia sana kuliko kitu chochote,na wengne ndugu zao.Mfano mm bila kumshirikisha kakaangu niliemnyanganya ziwa naona siwezi fanikiwa na ndoo msiri wangu.

Mshauri na kila ninalomshirikisha anaweza liboresha na likatoboa.Kwahiyo unavyosema hayo inategemea ndugu yangu na zaidi haya maisha hatuwezi kufanana kwenye mbinu za kuishi na kutatua shida zetu.
 
Hapo vipi..??

Mweka mada amekandia watu wanaotuzunguka na kusahau kuwa wewe mwenyewe unaweza kuwa mbaya wa maisha yako!!..

Kama akili haitoshelezi unafikiri nani atakaepata athari wa kwanza kwa akili hiyo..??

Kama utaendekeza uvivu,ujinga,ushetani na kila aina ya upuuzi hapo hauhitaji mtu mwengine awe adui wa maisha yako!.. isipokuwa wewe mwenyewe umeshakuwa adui wa maisha yako binafsi.

Kwangu mmbaya wangu wakwanza ni Mimi mwenyewe!!… Kabla haujashuku wenzio je wewe umejishuku..??
Kabla hujasema wenzio kuwa wananuka je,wewe umejihakiki haunuki..??

Ikiwa tutaweza kujisimamia uimara wa nafasi zetu basi hatutaona nani mbaya!.. nafasi ya kwanza ya ubaya kujishuku ianze nawe ya pili ije kwa wengine ila ujihakiki kuwa nawe huna ubaya..

Maisha sometimes hayanaga formula!.. haka ka kauli kapana!.. siku njema.
 
Kuna sehemu umezungumzia mapenzi, yani Yale yanayoleta zao la mtoto, Kuna sehemu unasema anaweza asikupende wewe ila akapenda tako lako au macho yako, Swali langu ni je? Hilo tako au macho ni viungo vya nani au vinapatikana kwa nani?

Je ni sehemu ipi ya mwili ikipendwa kwako utaamini ni kupendwa kweli. Angalizo kabla hujanijibu maswali yangu? Usiniletee habari za kwamba mtu anakupenda bila sababu. Naomba kuwakilisha
 
Kuna sehemu umezungumzia mapenzi, yani Yale yanayoleta zao la mtoto, Kuna sehemu unasema anaweza asikupende wewe ila akapenda tako lako au macho yako, Swali langu ni je? Hilo tako au macho ni viungo vya nani au vinapatikana kwa nani? Je ni sehemu ipi ya mwili ikipendwa kwako utaamini ni kupendwa kweli. Angalizo kabla hujanijibu maswali yangu? Usiniletee habari za kwamba mtu anakupenda bila sababu. Naomba kuwakilisha
Oooh kunamtu anaweza kupenda mwanamke ikiwa mwanamke anakalio kubwa kwa sasa wanaita wowowo na kuna mwingine anampenda mwananke kwa kila kitubalichonacho so hebu niambie kaka kati ya hao wawili ni nani atachokwa mapema?
 
Yani umeandika ukweli mtupu rafiki ni mtu mbaya sana, nina rafiki hapa tumefanya dili limezaa matunda kumbe rafiki anavuna mavuno ya dili kimya kimya nimekuja shituka ameshavuna 15M, ni rafiki ambaye alikuwa hajui chochote nimemshirikisha na kumfundisha leo amekuwa mnafiki namba mmoja.
 
Oooh kunamtu anaweza kupenda mwanamke ikiwa mwanamke anakalio kubwa kwa sasa wanaita wowowo na kuna mwingine anampenda mwananke kwa kila kitubalichonacho so hebu niambie kaka kati ya hao wawili ni nani atachokwa mapema?
mm siamini katika kupenda vyote, kiungo kimoja katika mwili wako kinaweza kuamsha hizia za mahusiano kwa mtu Fulani , na ukiwa nae huyo mtu aliyekuvutia labda tako haina maana humpendi.

Unampenda ila kupitia tako lake. Hivyo unaweza mpenda mtu kupitia Mambo mbalimbali Kama tako, macho, sura, shape, kimo, elimu, Mali, wadhifa, tabia nk.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom